Jovial avunja kimya kuhusu uhusiano wake na Willy Paul

Imebainika kuwa ilikuwa tu kiki ya wimbo ambao Pozee na Jovial walitoa

Muhtasari

• "Itoshe! Pozee si mpenzi wangu! Ni rafiki tu, ilikuwa biashara ambapo sote tulipata faida! Kwa sasa tumerudi kwa maisha yetu ya kawaida," Jovial alisema.

Willy Paul na Jovial
Image: Wily Paul Instagram

Msanii wa kizazi kipya nchini Kenya Jovial kwa mara ya kwanza amevunja kimya wake kuhusu minong'ono ya kuwa mpenzi wa Willy Paul.

Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Facebook, Jovial aliweka wazi kuwa Pozee si mpenzi wake.

Alikuwa ameulizwa maswali na mashabiki wake huku akiwajibu na wengi wao walitaka kujua kuhusu uhusiano wake na msanii huyo. 

"Je, Pozee ni mpenzi wako wa dhati?" mwanamtandao mmoja aliuliza.

Jovial alisema kuwa amechoka kujibu maswali ya watu kuhusu uhusiano wake na Willy Paul ndiposa akaamua kukomesha madai ya kuwa wanachumbiana.

"Itoshe! Pozee si mpenzi wangu! Ni rafiki tu, ilikuwa biashara ambapo sote tulipata faida! Kwa sasa tumerudi kwa maisha yetu ya kawaida," mwanamuziki huyo alisema.

Alisema aliamua kufichua hayo kwa kuwa ameshindwa kuvumilia maswali ya wanamitandao wakisukuma uhusiano wake na Poze kwa hatua nyingine.

"Nimekabwa na maswali yenu! Mungu anaisaidie kwa yatakayofuata! Aiii!Mayooo!" aliandika.

Mwanamuziki huyo pia aliulizwa iwapo anapanga kumleta mtoto wa Pozee duniani.

"Ndio, Nina uhakika unamaanisha 'na mpenzi wangu'," Joval alimjibu.

Hivi majuzi, wawili hao walikuwa wamethibitisha kuwa kwenye uhusiano baada ya Pozee kumtaka Jovial kuwa mpenzi wake.

Uhusiano wao hata hivyo ulishutumiwa na wanamitandao wengi ambapo wengi walisema kuwa uhusiano huo hautadumu na mwanamuziki Jovial atakuwa na majonzi baadaye. 

Hata hivyo, Jovial aliwasuta na kusema kuwa maneno ya wanamitandao hayatabadilisha uamuzi wake kuhusu mapenzi yake kwa Pozee. Willy Paul alikubaliana naye na kuwanyamazisha wanamitandao. 

"Hakuna kitu ambacho kitabadilika hata mkiongea,tushapendana na ni hivyo. Hii picha ya kifamilia iko aje?" Pozee alisema.