Wimbo wa Willy Paul warudishwa YouTube siku moja baada ya kutolewa

Wimbo wa Willy Paul umerudi YouTube baada ya kutoweka

Muhtasari

• Willy Paul bado hajaeleza sababu ya wimbo huo kupotea YouTube hata baada ya madai ya kuwa alikuwa amechukuwa wimbo wa mwanamuziki mwengine huku madai mengine yakisema yeye mwenyewe aliutoa wimbo huo ili kutafuta kiki.

Image: Willy Paul

Wimbo wa mwanamuziki Wilson Abubakar Radido almaarufu Willy Paul na Jovial uliokuwa umetoweka mtandaoni YouTube umerudi.

Wimbo huo ulikua umepotea kwa madai ya kuwa ulikuwa wa mtu ambaye alipeleka malalamishi ya hatimiliki kwenye wamiliki wa mtandao wa YouTube ndipo ukatoweka.

Wimbo huo wa kimapenzi sasa umefikisha 'views' zaidi ya laki nne baada ya kutoweka ukiwa na views elfu 5 pekee na ndio nambari 4 kwa kutamba.

Willy Paul amefahamisha mashabiki wake kwenye mtandao wake wa Instagram kuenda kwenye mtandao wa YouTube kuangalia wimbo huo na kuwa ni mzuri .

Mwanamuziki huyo, baada ya wimbo huo kurudi, alisema kuwa anamwabudu Mungu anayeishi na anayempenda sana .

"Hatimaye wimbo wa Lalala umerudi YouTube lakini hautambi. Endeleeni kuutizama wimbo huo ili tumjulishe shetani kua nimekingwa na damu ya Yesu na bado niko hapa sibanduki," alisema.

Jovial pia aliwafahamisha mashabiki wake kuwa wimbo huo umerudi kule YouTube ili waende kuuskiza wimbo huo.

Hii ni baada ya Willy Paul kufikisha wafuasi milioni moja YouTube ila mwanamuziki huyo bado hajashereheka hatua hiyo.

Wanamuziki hawa wawili waliutambisha wimbo wao kabla ya kuutoa kwa kutafuta kiki na kusema kuwa wako kwenye mahusiano.

Bado haijadhibitikaa kama bado wako kwenye mahusiano baada ya wimbo huo kurekodiwa na kuwekwa YouTube.

Willy Paul bado hajaeleza sababu ya wimbo huo kupotea YouTube hata baada ya madai ya kuwa alikuwa amechukuwa wimbo wa mwanamuziki mwengine huku madai mengine yalisema yeye mwenyewe aliutoa wimbo huo ili kutafuta kiki.

Mashabiki wake walimpongeza Willy Paul kwa kutoa wimbo huo uliovuma kabla na baada ya kupotea YouTube na kumkumbusha mwanamuziki huyo kuwa amefikisha wafuasi milioni moja kwenye YouTube.