Kudos! Eric Omondi awapongeza Jovial na Willy Paul kwa mahusiano

Omondi alisema kuwa amefurahishwa na wanachofanya wawili hao

Muhtasari

•Wengi walisema kwamba huenda kuna collabo mpya iliyokuwa inapikwa na wawili hao na ni kiki tu ya ufuasi walikuwa wanakimbiza katika mitandao ya kijamii mbele ya wimbo wao.

Image: Eric omondi Instagram

Mcheshi Eric Omondi awapongeza wanamuziki Wilson Abubakar Radido alimaarufu Willy Paul na anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa Juliet Miriam Ayub alimaarufu Jovial.

Omondi alisema kuwa amefurahishwa na wanachofanya wawili hao ambao wamekuwa wakianika mahaba yao kwa wiki sasa.

Wengi walisema kwamba huenda kuna collabo mpya iliyokuwa inapikwa na wawili hao na ni kiki tu ya ufuasi walikuwa wanakimbiza katika mitandao ya kijamii mbele ya wimbo wao.

Mcheshi Eric aliongeza na kuwashauri watu ambao wako kwa sekta ya sanaa na wanamuziki wazoee kuongeza chumvi na madoido kwenye kazi zao ili waweze kuwavutia watu.

“Muache kutuchosha na kutuboo, muwe watu wabunifu, muache kuwa watu wanaotabirika na wasiohitajika kisha mtaona matokeo na mtanishukuru baadaye!” alisisitiza.

Omondi alisema kuwa talanta iko kila mahali ikiwemo Tanzania na Nigeria kwa hivyo talanta peke yake si kitu kitakachoifanya sekta ya burudani na muziki kuwa kubwa miongoni mwa nchi hizo nyingine.

Alisema nchi hizo mbili alizotaja huitoa Kenya na kuwa zaidi yetu kwa sababu ya showbiz ambayo wanaanika kwa mashabiki wao. Omondi alifichua kuwa showbiz ndiyo itakayowapa wanamuziki hela kuliko kitu kingine chochote kwenye muziki.

Mcheshi huyo alisema kuwa hana uhakika kuhusu kinachoendelea baina ya Jovial na Willy Paul lakini wamemtumbuiza na mahaba hayo kwani ndiyo yatakayowasaidia kwenye muziki wao.

Hiki ndicho nilichokuwa ninaongelea,napenda hivi. Sijali na sijui nini inaendelea hapa lakini hii ni showbiz tupu na naipenda.Kudos Willy Paul na Jovial, kama ni wimbo ama mnashiriki matendo ya mapenzi,” alisema.

Omondi alitoa mfano wa mwanamuziki wa Tanazania, Diamond na kusema mwanamuziki huyo hupata hela kutokana na kutumbuzia mashabiki wake na showbiz.

Aliwashauri wanamuziki na wanaburudani kutafuta kiki ipasavyo kwani hiyo ndiyo itakayowaongezea mashabiki na kuwalipa vinono.