"Hata rais Ruto alianza kwa kuuza kuku" - Willy Paul awajibu wanaokejeli biashara yake

Willy Paul wiki jana alizindua gari lake ambalo alisema liko tayari kwa kukodisha na kuwa ndio biashara yake mpya.

Muhtasari

• Walisema Pozze sio mtu mwenye akili za kibiashara, nani anacheka sasa? - Paul.

Willy Paul awajibu wanaokejeli biashara yake ya matatu
Willy Paul awajibu wanaokejeli biashara yake ya matatu
Image: Instagram

Mwanamuziki Willy Paul siku chache zilizopita alizindua biashara yake mpya ya kukodisha magari. Alitangaza haya alipokuwa kwenye mahojiano na Mungai Eve - akifichua kuwa ana matatu mpya ambayo watu wanaweza kukodi wakati wa safari za barabarani, harusi na hata mazishi.

Watu mbali mbali walimhongera kwa biashara hiyo mpya huku wengine walimsuta kwamba gari hilo ni zee, haswa baada ya mkurugenzi mkuu wa kampuni ya utalii ya Bonfire, Simon Kabu kupakia picha akisema kwamba gari hilo lilikuwa la kampuni yake awali kabla ya kulipiga mnada.

Hata hivyo kwa Diman Mkare mmoja, mwanamitindo na mvulana ambaye sote tulidhani alikuwa marafiki na Pozee alihisi wazo zima la matatu halikufaa. Kwake, kufanya hatua kubwa kama vile kununua choppers ndicho Pozee anapaswa kuzungumzia. Akizungumza na SPM buzz, Diman Mkare alimkejeli Willy akisema kwamab wasanii wa haiba yake wanafanay mambo makubwa ilhali yeye ananunua matatu zilizotumika hadi zikachoka mwendo.

“Wasanii wakubwa wananunua helikopta na wewe hapa  unaenda kwa matatu? Hivi sasa, Willy Paul ni msanii mkubwa, anapaswa kuzindua mambo makubwa, sio matatu,” Mkare alimkejeli.

Msanii Rayvanny pia kutoka Tanzania wikendi iliyopita aliandika maneno kwenye instastory yake akionekana kumkebehi Willy Paul ambapo alisema kwamba anasikia watu wana matatu mjini.

Pozee baada ya kushindwa kumeza haya yote, aliamua kujibu mipigo ambapo alisema kuwa watu wanafaa kuheshima hatua zake chonde chonde kwani hata rais wa Kenya William Ruto hakuamka tu na kujipata tajiri bali alianza kwa hatua za chini kama mkulima wa kuku.

“Ndugu zangu asanteni sana kwa kuja. Nina deni lenu... walisema Pozze sio mtu mwenye akili za kibiashara, nani anacheka sasa? Baada ya kuomba kwa muda mrefu sana, Mungu anipe wazo la biashara... Hatimaye akafanya na nikachukua wazo hilo na kulipatia uhai... #matyapozze anapatikana kwa kukodi wasiliana na @saldido_international kwa maelezo zaidi.. Kwa mara nyingine tena kubwa asanteni wote kwa maombi yenu... ata mheshimiwa rais alikuwa anauza kuku... twende!” Pozee alipiga mizinga.

Willy Paul awajibu wanaokejeli biashara yake ya matatu
Willy Paul awajibu wanaokejeli biashara yake ya matatu
Image: Instagram