Jaribuni bahati yenu! Pozee kwa wanawake wanaomtaka

Pozee aliwambia wanawake wamtumie ujumbe iwapo wangetaka kuwa kwenye uhusiano naye

Muhtasari

• Wanamitandao wengi wamekisia kuwa Pozee anatafuta kiki kwa wimbo wake unaokuja na kumwambia kuwa amefanikiwa kupata umakini wao.

Willy Paul
Image: Willy Paul Instagram

Mwanamuziki Willy Paul amewashauri wanawake wanaotaka kuwa kwenye uhusiano naye kujaribu bahati .

Kwenye Instagram, Pozee aliwaambia wanawake wanaotamani kuwa naye kimapenzi kumtafuta na kumtumia jumbe kwani wanaweza kubahatika kuwa naye.

"Ili kupata mpenzi mtanashati na mwenye talanta kama mimi, nitumie ujumbe. Jaribu bahati yako leo usingoje kesho," Pozee alisema.

Wanamitandao wengi wamehisi kuwa Pozee anatafuta kiki kwa wimbo wake mpya na kumwambia kuwa amefanikiwa kupata umakini wao.

Walimwambia kwamba sasa anaweza kuachia wimbo huo.

Wengine hawakufurahia kwani walisema mwanamuziki huyo anatumia tu wanawake kutafuta kiki huku wengine wakiuliza iwapo uhusiano wake na mwanamuziki Jovial ulikuwa wa kutafuta kiki.

"Unawashtua sana watu, pozee ndio jina hii Kenya,"hey_its_moose alisema.

"Hakuwezi kosa aliyetuma,"naff_iruri alisema.

"Kwani Jovial amefanya nini?" _reihna aliandika.

Hivi majuzi, Pozee aliwashauri wanaume ambao wako kwenye uhusiano kutowabembeleza wanawake.

Aliwaambia wanaume kuwa iwapo mwanamke wanayechumbiana anataka kuondoka kwenye uhusiano wamruhusu tu.

"Wanaume wenzangu, iwapo mwanamke anataka kuenda muache aende. Ni wengi wanaokungoja na kukutaka. Kama wewe ni mwaminifu kwake na bado hakuamini basi mwache aende asubuhi na mapema kabla jua liwake," Pozee aliandika.

Willy Paul pia alitangaza kwamba ataanza mchakato wa kuafuta marafiki kwenye mtandao wa Instagram ambao wana roho mbaya na akili potovu.

Pozee alitangaza haya kupitia Instagram story yake ambapo alisema kwamba kama wewe ulikuwa rafiki yake na utaona ameku unfollow basi ujue ni miongoni mwa watu wale ambao amewaorodhesha kama wenye akili potovu kwake.

“Kwa hiyo leo nitakuwa nawa-unfollow watu wenye fikira potovu. Ikitokea nimeku-unfollow, tulia tu na ujikusanye na kuendelea na maisha yako…lakini bila mimi,” Willy Paul aliandika huku akimalizia kwa emoji za kucheka.