Mamake Colonel Mustafa afunguka kuhusu vita vyake na ugonjwa wa saratani

Alisema mwanzoni hakudhani ni ugonjwa wa kutishia kwa kuwa alikuwa na shida ya Ulcers.

Muhtasari

• Mama yake Mustafa alianza kwa kuelezea kuwa alianza kuumwa kidogo mnamo mwaka wa 2021. 

•Daktari alipofanya vipimo akapata kuwa figo yake mama imeathirika sana na ugonjwa huo wa saratani.

Mamake Colonel Mustafa alisimulia huku akiwa amejawa na machozi safari yake jinsi amekuwa akipambana na ugonjwa wa saratani.

Katika mahojiano na Mungai Eve, mamake Mustafa alianza kwa kuelezea kuwa alianza kuumwa kidogo mnamo mwaka wa 2021. Hata hivyo, hakudhani ni ugonjwa wa kutishia kwa kuwa alikuwa na shida ya Ulcers. Alipoenda hospitali alipewa dawa kisha baada ya kuzimeza na kupata nafuu kidogo anawacha kuzimeza.

Aliongezea na kusema kuwa baadaye maumivu yalizidi kuanzia Januari 2022 na hata akienda hospitali alikuwa anaambiwa na daktari kuwa mara anaugua malaria , mara UTI.

"Baadaye nikazidiwa, dadangu akanipeleka hospitali, kwanza kabisa nilikuwa nadhani nina saratani ya kizazi kisa na maana ugonjwa ulihama ukakuja ikawa ninaumwa sehemu ya kizazi sana.

Hivyo basi,nikaenda hospitali kupimwa cancer kule Tanzania ila baada ya kupimwa hadi matiti daktari akaniambia sina saratani  nikaambiwa niko sawa lakini sasa nikauliza ni nini  kinanisumbua?

Daktari yule aliniambia kuwa huenda ikawa ni kizazi kinakusumbua nikaenda nikafanyiwa ultrasound majibu ndio nikaambiwa kuwa figo yangu ndio ina maji na kuwa UTI ndio umesababisha na pia huwa unaathiri figo. 

Kisha nikapewa dawa nikazitumia kama mwezi mmoja  lkn maumivu bado yako. Kurudi hospitali na kufanyiwa ultrasound niliambiwa kuwa figo zina mawe," Mamake Mustafa alieleza huku akilia.

Mamake Mustafa alisema wanawe walisisitiza atoke Tanzania akuje Kenya ila alikataa na kuamua kuenda kumwona daktari wa figo. Daktari yule alimpa ushauri na kumpa dawa za kuondoa maumivu ila hapo ndipo alipozidiwa hadi afya ikadhoofika.

Mama yule akamwambia dadake wabadilishe daktari kwa kuwa hali yake ilikuwa mbaya hivyo dadake alimpigia rafiki yake ambaye aliwasaidia kupata nambari ya daktari ambaye ni bingwa wa figo.

"Tukampigia simu daktari yule wa figo akasema kuwa yeye hayuko Tanzania labda tusubiri baada ya wiki moja na mimi hiyo wiki moja nilikuwa naona ni kama ni mwaka kumi maanake maumivu nilikuwa nayo silali usiku wala mchana sana nlkuwa na kilo 96 zikapungua kiasi sababu sili natapika.

Daktari yule alipokuja Jumatatu tukaenda na zile dawa ila daktari yule hakuzizihitaji kwa kuwa  hajui ni nn kinanisumbua. Daktari huyo akanituma niende kwa CT Scan nikaonekana kuwa nimeathirika kwenye mgongo na kuna uvimbe ambao umetapakaa mpaka sehemu ya figo kwani umekula figo, umekula ini kidogo na  umekula mishipa miwili ya damu na mgongo," alielezea mama huyo.

Mama huyo alisema kuwa hapo ndipo dadake alimkatia tiketi ya ndege ya kumfikisha hadi Kenya kwa maana hakuwa anaweza kuketi chini na akaweza kufika Kenya usiku huo.

Alieleza kuwa kesho yake Daudi alimpeleka hospitali ila daktari baada ya kuangalia karatasi ile ya CT Scan aliwashauri waende hospitali ya Kijabe.

Siku ya Jumatatu wakaelekea hiyo hospitali na kuweza kupeana sampuli ya damu yake ndio iweze kupimwa. Baada ya wiki mbili majibu yalitoka na wakaambiwa kuwa ana ugonjwa wa saratani ila anawezakusaidika.

Kisha wakatafuta daktari shabaha wa cancer na baada ya kumpata na kupimwa walipata kuwa figo yake mama imeathirika sana na ugonjwa huo wa saratani.

"Baada ya wiki mbili daktari alipima kuangalia kama mapafu na ini yangu yanaweza yakaimili dawa hiyo ya cancer ikakuwa niko vizuri kidogo ndio nikaanza matibabu. Hapo ndipo nilipoanza kuimarika kidogo nashukuru Mungu.

Haswa yale maumivu kupungua mpaka nikaweza  kulala hiyo ni hatua moja kubwa sana na nashukuru mungu Alhamdulillah," Mama Mustafa alinena