"Ni kuvumiliana tu!" Bahati alalamika kuhusu tabia ya mkewe Diana Marua ya kunyamba

Bahati alidokeza kuwa hiyo ni shida ambayo amekuwa akiishi nayo kwa miaka saba iliyopita ya ndoa yao.

Muhtasari

•Bahati alishiriki video ya burudani ambapo Diana alionekana akiigiza kunyambwa wakati wakiwa wamelala pamoja kitandani.

"Siku hizi tunaporudi nyumbani kutoka kwenye karamu, dakika anapoingia mlangoni anaanza kunyamba," Bahati alisema.

Diana Marua na mumewe Bahati
Diana Marua na mumewe Bahati
Image: Screengrab

Mwanamuziki Kelvin Kioko almaarufu Bahati amekejeli tabia ya mkewe Diana Marua ya kunyamba wakati wakiwa pamoja .

Siku ya Alhamisi, mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alishiriki video ya burudani ambapo Diana alionekana akiigiza kunyambwa wakati wakiwa wamelala pamoja kitandani.

"Ulipozoea kuamka na ujumbe mzuri wa asubuhi sasa unaamka na hii (kunyamba)," maelezo ya video iliyochapishwa na Bahati yalisomeka.

Baba huyo wa watoto wanne alidokeza kwamba hiyo ni shida ambayo amekuwa akiishi nayo kwa miaka saba iliyopita ya ndoa yao.

“Miaka 7 ya ndoa nikuvumiliana tuu,” aliandika.

Haya yanajiri takriban miezi miwili tu baada ya mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi kufichua kuwa mke wake Diana Marua hakuwahi kunyamba mbele yake kwa miaka miwili ya kwanza ya ndoa yao.

Kwa wanandoa wengi, tabia kama vile kunyamba na kwenda chooni wakati mwenzio anatazama inamaanisha kuwa mnafurahia ndoa yenu.

Kupitia chaneli ya YouTube ya Diana Marua, mwimbaji huyo wa kibao ‘Mama’ alifichua;

"Tulipoanza kuchumbiana hakuwahi kunyamba mbele yangu kwa miaka miwili ya kwanza. Siku hizi tunaporudi nyumbani kutoka kwenye karamu, dakika anapoingia mlangoni anaanza kunyamba.

Siwezi kuendelea kufanya mapafu yangu kuteseka. Ulichokuwa ukifanya ni kunyunyizia kisafisha hewa kwanza kabla ya kuendelea kufanya 'biashara' yako." Alilalamika Bahati.

Wakati huo, Bahati alidokeza kwamba wanawake hawapaswi kuzingatia kuonekana wazuri kwa watu wengine na sio kwa wapenzi wao.

"Sijawahi kuelewa kwa nini wanawake akiwemo Diana wanataka kuwa warembo mbele ya kamera lakini nyuma ya kamera, hawaonekani wazuri. Tukifika nyumbani kitu cha kwanza anachofanya ni kutoa wigi, kutoa make up na kurudi kwangu akifanana na DJ Shiti. Ikiwa unataka kukaa vizuri, usisubiri tu wakati unatoka. Pia nataka kukuona wewe ukiwa mrembo,” Bahati alisema.