Mrembo bikira mwenye umri wa miaka 34 alia kutopata mume licha ya kulinda usichana wake

“Kwa kweli sikufikiria ningefikisha miaka 34 nikiwa bado bikira kwa sababu nilifikiri ningekuwa nimeolewa na mume wangu na kufanya mambo ya kutengeneza vitumbo," alisema.

Muhtasari

• Mrembo huyo kwa daili zote alionesha dalili za ulokole na uchamungu kwa kiasi cha haja.

Zukiswa Joyi, bikira wa miaka 34.
Zukiswa Joyi, bikira wa miaka 34.
Image: Facebook

Mrembo mmoja kutoka Afrika Kusini kwa jina Zukiswa Joyi ambaye mwaka jana hadithi yake ilisimuliwa katika jarida la Vaguard Online News kama mmoja kati ya wasichana wachache ambao wamelinda usichana wao hadi Zaidi ya umri wa miaka 30 sasa amerejea mwaka huu akilia kutopata mume.

Joyi kupitia ukurasa wake alikuwa anasherehekea kufikisha umri wa miaka 34 akisema kuwa bado yeye ni bikira na hajawahi onana kimwili na mwanamume mwingine.

Alionesha kusikitishwa kwake kwamba licha ya kulinda usichana wake, bado hajapata mume wa kumuona na hilo limemfanya kuendelea kuishi katika ulimwengu wa kusadikika kuhusu masuala ya mapenzi na ndoa kwa jumla.

Joyi alisema kwamba alikua, alikuwa anadhani kwamba hatokuwa bila mume akiwa na umri wa miaka 34 lakini sasa ndio ukweli mchungu unamgonga usoni kwamba atahitaji kusubiri Zaidi ili kumpata mmoja anayemfaa.

“Kwa kweli sikufikiria ningefikisha miaka 34 nikiwa bado bikira kwa sababu nilifikiri ningekuwa nimeolewa na mume wangu na kufanya mambo ya kutengeneza vitumbo lol lakini ke, kama Bwana angekuwa nayo hapa kwetu.” Alisema.

“Wamesimama tu kwa sababu ya neema yake kwa sababu hakuna saa ya kibayolojia na kalenda ya matukio iliyoundwa dhidi yetu itafanikiwa sisi ni watu wa Imani na tunamwamini yule ambaye zaidi ya wakati na ni mzee wa siku, hii inaweza tu kuwa kazi ya Roho Mtakatifu. Ninaendelea kuzeeka kwa uzuri kama divai nzuri,” alijiliwaza.

Joyi ambaye kwa daili zote alionekana kama mchamungu wa kutolewa mfano hai alisimulia kwamba kilichomfanya kulinda usichana wake kwa miaka hiyo yote ni kuwa ametoka na kulelea katika mazingira na familia ya kilokole ambayo ilikuwa ni mwiko kushiriki mapenzi kabla ya ndoa.