Bi Harusi afichua mume mtarajiwa alipata namba yake kutoka kwa MC wakiwa chuoni

“MC ni best friend wangu kuanzia chuoni na wote tulikuwa marafiki wa Polycarp [Bwana Harusi] na Polycarp alichukua namba yangu kutoka kwa Teresia [MC]. Kwa hiyo Teresia ndio aituunganisha,” Bi Harusi alisema.

Muhtasari

• MC alijipiga kifua na kuwaambia wanaotafuta wapenzi kuishi vizuri na yeye.

Bwana na Bibi Harusi.
Bwana na Bibi Harusi.
Image: Screengrab

Bibi harusi mtarajiwa amewashangaza wengi wakati wa hafla ya harusi yake baada ya kufichua kwamba MC wa sherehe hiyo yao ambaye ni rafiki wake wa kutoka utotoni waki shule ndiye aliyempa mume mtarajiwa namba yake ya simu.

Katika video hiyo ambayo imepakiwa na MC huyo kama njia moja ya kijitangaza kwa huduma nzuri, alianza kwa kumpa Bibi harusi nafasi ya kuwahutubia watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo la kumpendeza Mungu.

Bibi harusi alianza kwa kumsifia MC huyo wa kike na kusema kwamba bila yeye [MC]  hakungekuwa na harusi hiyo kwani ndiye aliyecheza nafasi kubwa kuhakikisha kwamba wawili hao wamejuana na kuanza uhusiano ambao uliishia kwa harusi ya kanisani.

“MC ni best friend wangu kuanzia chuoni na wote tulikuwa marafiki wa Polycarp [Bwana Harusi] na Polycarp alichukua namba yangu kutoka kwa Teresia [MC]. Kwa hiyo Teresia ndio aituunganisha,” Bibi harusi alisema huku akichekacheka kwa aibu ya kufichua siri hiyo.

Kwa upande wake, bwana harusi alisema kwamba baada ya kupata namba ya mkewe kutoka kwa MC kipindi hicho wakiwa chuoni, haikuwa rahisi kwake kupata ndio yake katika mahusiano.

“Teresia nilimwambia, mbona yule dada ulinipa namba yake mbona hajibu meseji zangu? Akampigia simu akamwambia mbona hujibu meseji za yule kaka wa ofisini? Akasema aah kumbe ndio yule, na hapo ndipo ali’save namba yangu “kaka wa ofisini” na tukaanzia hapo,” bwana harusi alisema kwa aibu vile vile.

MC Huyo baada ya kumiminiwa sifa kama chanzo cha harusi hiyo, aliwambia watu kwa utani haswa wale wanaotafuta wapenzi kuishi vizuri na yeye.