Ex wa Baha, Georgina Njenga atuma onyo kali kwa msichana aliyemnyakua mpenzi wake

Mpenzi wa zamani wa Baha, Bi Georgina Njenga ametuma onyo la kejeli kwa msichana ‘aliyemwibia’ mpenzi wake.

Muhtasari

•Georgina alichapisha video inayomuonyesha akiimba wimbo wa Alikiba na Marioo ‘Sumu’, sehemu ambayo wanaimba kuhusu watu kukutana tu kwani wao si milima.

•Haya yanajiri siku chache tu baada ya mtayarishaji huyo wa maudhui kuweka wazi kuwa yeye bado hana mpenzi lakini hatafuti. 

Georgina Njenga
Georgina Njenga
Image: Instagram

Mtayarishaji wa Maudhui na mshawishi wa mitandaoni maarufu wa Kenya Georgina Njeri Njenga ametuma onyo la kejeli kwa msichana ‘aliyemwibia’ mpenzi wake.

Siku ya Ijumaa, mpenzi huyo wa zamani wa muigizaji Tyler Mbaya, kwa jina maarufu ‘Baha’ alichapisha video inayomuonyesha akiimba pamoja wimbo wa Alikiba na Marioo ‘Sumu’, sehemu ambayo mastaa hao wa bongo fleva wanaimba kuhusu watu kukutana tu kwani wao si milima.

“Sisi sio milima, tutakutana. Sisi ni watu, tutaonana. Sisi sio milima, tutakutana. Tukiwa kama watu, tutaonana,” Georgina aliimba pamoja na Alikiba na Marioo.

Katika sehemu ya maelezo ya video hiyo, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kuwa maneno ya wimbo huo yalielekezwa kwa msichana aliyemchukua mpenzi wake.

"Kwa msichana ambaye alimnyakua mtu wangu ..." aliandika.

Hata hivyo hakufafanua ni mwanamume yupi ambaye alikuwa akimzungumzia wala msichana aliyemchukua.

Image: INSTAGRAM// GEORGINA NJENGA

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mtayarishaji huyo wa maudhui kuweka wazi kuwa yeye bado hana mpenzi lakini hatafuti. Alifichua hayo wakati wa mahojiano na mwanahabari Nicholas Kioko baada ya kuhojiwa kuhusu hali ya uhusiano wa aliyekuwa mpenzi wake, Tyler Mbaya.

Mama huyo wa binti mmoja alibainisha kuwa hawezi kujua ikiwa mzazi mwenzake, Tyler Mbaya amesonga mbele na maisha yake au la, lakini pia akathibitisha kuwa yeye yuko peke yake lakini hatafuti mpenzi.

"Sijui kama amemove on lakini mimi niko soko...bado sijapata mpenzi lakini sitafuti... Niko soko kujitafuta, na kugrow," alisema.

Georgina pia alifafanua kuwa chapisho lake la hivi majuzi kuhusu kuchumbiana na mwanamume asiye tajiri lilitafsiriwa vibaya na watu lakini akaeleza kuwa hatajali kukua na mwanaume.

"Kwa kweli lilikuwa swali. Naamini katika kufanya kazi kwa bidii, na ninaamini kabisa kukua na mtu. Siamini kwamba kulipa bili ni jukumu la jinsia. Ama kama msichana nafaa kuwa na mtu mwenye ananitumia kiasi fulani. kwa mwezi. Ikibidi uifanye kwa sababu ya kufanya, ifanye kwa sababu unanipenda," Alisema.

Alisema zaidi kwamba alitamani maisha yake na baba ya mtoto wake.

"Ndio kweli lakini maisha yalitokea, mambo yalitokea hivyo tunaendelea. Kitu kimoja cha maisha ni maisha yanasonga mbele, maisha yanaendelea hivyo hata nikimmiss, hizo ni kumbukumbu na angalau Astara atakua anasema tulikuwepo."

Georgina pia alifichua kwamba mipango ya baadaye ya uhusiano wake na Tyler haijulikani lakini akabainisha kuwa sura hiyo haikufungwa kabisa.

"Nadhani ningesema hujui na maisha. Huwezi pangia life. Leo naeza kuwa nimeplan hatutarudiana alafu turudiane ama niseme hapa hatuezi rudiana nayeye alafu turudiane. Ama niseme tunaeza rudiana alafu tukose. But of cause, destiny holds its place so maybe its place so maybe rudiana nayeye alafu turudiane. siku moja.

Kama vile sina mpango kuhusu maisha yangu. Nita panga ndio lakini Mungu ndio ako na ufunguo mkuu kwa hivyo labda ndio, labda hapana, lakini ni kitu ambacho sijafunga kabisa kutoka kwa sura yangu," Georgina alisema.