Georgina Njenga akiri kuna uwezekano wa kurudiana na Ex wake, Baha Machachari

“…kurudiana [na Baha Machachari] si kitu ambacho naweza sema nimekifungia nje kabisa ya ratiba ya maisha yangu. Hapana, kwa hiyo siwezi mind,” Georgina aliweka wazi.

Muhtasari

• TikToker huyo alisema kwamba hata kama ataratibu maisha yake lakini nafasi kubwa ya maisha hayo yake huwa anaiacha katika mikono ya Mwenyezi Mungu .

• "Kwa hiyo ninaweza sema kwamba alikuwa kama mpenzi wangu wa kwanza, kama ninafikiria vizuri."

BAHA NA GEORGINA
BAHA NA GEORGINA
Image: INSTAGRAM

Georgina Njenga, mpenzi wa zamani wa muigizaji Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari amekiri kwamba kuna uwezekano wa kurudiana naye katika siku za usoni kwa ajili ya mtoto wao.

Njenga alifichua haya katika mahojiano ya kipekee na YouTuber Nicholas Kioko na kusema kwamba hawezi futilia mbali kabisa uwepo wa Baha katika maisha yake kwani tayari wana mtoto pamoja na hicho ndicho kigezi cha muunganiko wao katika maisha yao yote.

 Mrembo huyo mama wa mtoto mmoja alisema kwamba katika maisha yake, yeye huendeshwa na falsafa kwamba huwezi kutabiri kutakachotokea katika maisha ya kesho, haswa akizingatia kwamba wawili hao tayari wana mtoto pamoja.

“Nafikiri naweza sema kwamba huwezi jua na maisha. Ni kama huwezi pangia maisha. Leo ninaweza kuwa nimepanga kwamba hatutarudiana halafu turudiane. Ama niseme hapa hatutarudiana halafu turudiane, au pia naweza sema hapa tutarudiana halafu tusirudiane. Lakini ukweli ni kwamba hatima ina nafasi yake, kwa hiyo pengine ipo siku. Mii huwa sina ratiba ya maisha yangu,” Georgina Njenga alisema.

TikToker huyo alisema kwamba hata kama ataratibu maisha yake lakini nafasi kubwa ya maisha hayo yake huwa anaiacha katika mikono ya Mwenyezi Mungu akiamini kwamba kesho yake i mikononi mwake.

“…kurudiana [na Baha Machachari] si kitu ambacho naweza sema nimekifungia nje kabisa ya ratiba ya maisha yangu. Hapana,” Georgina aliweka wazi.

Akiulizwa atakachokitaka endapo watafanikiwa kurudiana, Mrembo huyo alicheka na kusema;

“Ninataka chochote ambacho Mungu ataona ni mgao wangu, chenye Mungu ameamua ndicho hicho, siwezi mind.Mimi na Baha hatujawahi kosana ile eti hatuongei kabisa ama nikae nimuongelelee vibaya.”

Mrembo huyo alilaumu kutokomaa kwao kuwa kitu kilichochochea kuvunjika kwa penzi lao, akisema sasa kwa vile wote kama vile wamekomaa, huenda kila kitu kikawa sawa.

“Tulikuwa katika uhusiano ambao ulikuwa wa hadharani na pia tulikuwa wadogo. Mimi nilikuwa na miaka 18, kwa hiyo hatukuwa tunajua mengi, na kadri unavyokua ndio jinsi unavyojua mengi. Kwa hiyo ninaweza sema kwamba alikuwa kama mpenzi wangu wa kwanza, kama ninafikiria vizuri. Kwa hiyo siwezi sema kwamba alikuwa mtu mbaya kwangu. Tulikuwa tunakua na kujifunza ikafika mahali tukaona haiwezekani. Kwa hiyo chochote kile ambacho Mungu amepanga acha kiwe tu hivyo,” aliongeza.