"Acheni msichana afurahi!" Vera amtetea Betty Kyallo kuhusu kuchumbiana na kijana mdogo

.Kauli ya sosholaiti huyo ilikuja saa chache tu baada ya Betty Kyallo kumtambulisha mpenzi wake Charlie

Muhtasari

•Vera alibainisha kwamba wanamtandao bado walimkosoa Betty alipokuwa akichumbiana na wanaume wenye umri mkubwa katika siku za nyuma.

•Vera amewataka watu wakome kumshambulia mtangazaji huyo na kumwacha afurahie uhusiano wake kwa amani

ametetea mahusiano ya Betty Kyallo
Vera Sidika ametetea mahusiano ya Betty Kyallo
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika amemtetea mtangazaji wa TV Betty Kyallo kufuatia mashambulizi ya hivi majuzi kuhusu yeye kutoka kimapenzi na kijana mdogo.

Siku ya Ijumaa, Betty alimfichua mpenzi wake mpya kwa ulimwengu baada ya muda mrefu wa tuhuma na uvumi kutoka kwa wanamtandao. Kufuatia hatua yake, watumiaji wa mitandao ya kijamii waliweza kugundua tofauti ya umri inayoonekana kati ya wapenzi hao wawili huku mtangazaji huyo wa TV akionekana kuwa na umri mkubwa kuliko mpenzi wake Charlie, hii iliibua ukosoaji kutoka kwa sehemu ya watumiaji wa mtandao.

Huku akimtetea siku ya Ijumaa, Vera alibainisha kwamba wanamtandao bado walimkosoa Betty alipokuwa akichumbiana na wanaume wenye umri mkubwa katika siku za nyuma. Kufuatia hilo, aliwataka watu wakome kumshambulia mama huyo wa binti mmoja na kumwacha afurahie uhusiano wake kwa amani.

Mpeeni Betty mapumziko. Alipotoka kimapenzi na wanaume wakubwa wote mlikuwa bize kusema aibu kwake kwa kutoka na wababa na wanaume waliooa. Sasa kuchumbiana na kijana ni shida, eeh binadamu!! Acheni msichana afurahi," Vera alisema.

Kauli ya sosholaiti huyo ilikuja saa chache tu baada ya Betty Kyallo kumtambulisha mpenzi wake Charlie kwa ulimwengu kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Mtangazaji huyo wa TV alichukua hatua hiyo usiku wa kuamkia Ijumaa wakati akimsherehekea mpenzi wake mnamo siku yake ya kuzaliwa.

Katika ujumbe wake kwa mpenzi wake, Betty Kyallo alimtakia mambo mema na kwa uhusiano wao.

"Heri ya kuzaliwa mpenzi. Vicheko zaidi, furaha zaidi, kukumbatiana zaidi, watoto zaidi, sisi zaidi. Ni hivi,” Betty Kyallo aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha nzuri yake na mwanaume huyo. Pichani, mwanamume huyo anaonekana kuwa mrefu zaidi na ana rasta kichwani.

Mama huyo wa binti mmoja aliendelea kumshukuru mpenzi wake na kusherehekea mapenzi yao.

"Asante kwa kila kitu. Heri ya kuzaliwa,” aliandika.

Kyallo alijigamba kwa kujipatia mwanamume anayefaa na kuwapuuza kila mtu mwingine.

“Mungu alinitumia aliye sahihi. Nyinyi nyote mnaweza kuwa na hasira,” alisema.

Pia alijigamba kuhusu kuwa na furaha na mpenzi wake mpya na kumtakia mwanaume huyo mafanikio zaidi.

"Naomba mtu wangu ashinde kila wakati. Anashinda lakini nataka ashinde mengi zaidi. Juu ya Mungu. Furaha mke, maisha ya furaha,” alisema.

Hatua hiyo ya mtangazaji huyo mrembo imezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya wanamtandao wakiwapongeza na kuwatakia kila la heri huku wengine wakiibua madai kuwa mwanamume huyo ni mdogo sana kwa Kyallo.

Huku akijibu madai ya mpenzi wake kuwa na umri mdogo sana kuliko yeye, mama huyo wa binti mmoja alisema, "Hata hivyo, angalau miaka imeongezeka. Nina furaha. Wacha tusukume. Mambo ni deadly deadly.