"Alikuwa akinila!" Diamond Platnumz afichua mwanamke aliyempa busu bora zaidi

Staa huyo wa Bongo alibainisha kuwa busu la Fantana lilikuwa zaidi ya busu.

Muhtasari

•Diamond Platnumz alionekana akibusiana kimahaba na mwanamuziki wa Ghana Francine Koffie almaarufu Fantana.

•Diamond aliweka wazi kuwa busu la malkia huyo wa Ghana lilikuwa bora zaidi kuwahi kupokea katika miaka yote 32 ya kuwepo kwake.

amefichua kwamba busu la Fantana ndilo bora zaidi amewahi kupata.
Diamond amefichua kwamba busu la Fantana ndilo bora zaidi amewahi kupata.
Image: HISANI

Filamu ya maisha halisi ya Young, Famous and African  kwenye mtandao wa Netflix imeendelea kuibua tamthilia na matukio mapya katika maisha ya  baadhi ya watu maarufu wa Afrika katika tasnia ya burudani.

Sehemu ya pili ya filamu hiyo iliyosubiriwa kwa hamu  iliachiwa Ijumaa na vijisehemu vya baadhi ya vipindi tayari vimeonyeshwa.

Katika moja ya matukio kwenye filamu hiyo, staa wa bongo Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz anaonekana akibusiana kimahaba na mwanamuziki wa Ghana Francine Koffie almaarufu Fantana.

“Nilijiona mimi ndiye bora kwa kubusu, hadi nilipombusu Fantana,” Diamond alisema kuhusu tukio hilo la kubusiana.

Alibainisha kuwa busu la Fantana lilikuwa zaidi ya busu.

"Hakuwa ananibusu, alikuwa akinila!" alisema.

Diamond aliweka wazi kuwa busu la malkia huyo wa Ghana lilikuwa bora zaidi kuwahi kupokea katika miaka yote 32 ya kuwepo kwake.

Fantana ni mwimbaji na mwanamitindo wa Ghana ambaye pia ni mmoja wa wahusika wa kipindi cha ukweli cha Young, Famous and African. Hata hivyo hana historia ya uhusiano na Diamond mbali na kuwa washiriki wa YFA2.

Wahusika wengine wa filamu hiyo iliyojaa drama tele ni pamoja na mzazi mwenza wa Diamond Zari Hassan, rapa Nadia Nakai, muigizaji Khanyi Mbau, Naked DJ, Swanky Jerry, Kayleigh Schwark, 2Baba na Annie Idibia.

Siku ya Ijumaa, mpenzi wa zamani wa Diamond, Zari Hassan alikuwa na maelezo ya kumfanyia mumewe mdogo, Shakib Cham Lutaaya  baada ya kupeperushwa kwa sehemu ya pili ya filamu hiyo mapema siku hiyo.

Ninaelekea nyumbani kwa mume wangu kuelezea ni nini hicho kilikuwa  katika #YFA," Zari alitangaza kwenye mtandao wa Instagram siku ya Ijumaa jioni na kuambatanisha na video iliyomuonyesha akiendesha gari.

Mama huyo wa watoto watano alisikika akiimba kwa sauti kubwa kwenye video aliyoichapisha.

Haijabainika kama Zari alienda kumwomba radhi Shakib kutokana na kukabiliana kwake na Diamond kwenye filamu hiyo, kufufuliwa kwa kumbukumbu za mahusiano yao au nini hasa, lakini ni wazi alikuwa na mambo ya kumueleza mumewe huyo wa miaka 31.  YFA2 inahusisha maigizo, kufunguka, makabiliano baina ya wahusika kati ya mambo mengine yanayoweza kuvunja ndoa au mahusiano.