Dadake Diamond aolewa tena baada ya kugura ndoa ya awali miezi mitatu baada ya harusi

Esma na Jembe One wamekuwa wakichumbiana kwa miezi kadhaa kabla ya kufanya rasmi muungano wao Alhamisi jioni.

Muhtasari

•Esma na Jembe One almaarufu Cheedy walifunga ndoa siku ya Alhamisi jioni katika hafla ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na familia na marafiki.

•Ndugu za Esma wakiongozwa na Ricardo Momo na Queen Darleen kisha walionekana wakimzuia Jembe kuingia ndani hadi atoe kiasi fulani cha pesa.

Esma Platnumz na mume wake Jembe One
Image: INSTAGRAM// JEMBE ONE

Dada wa staa wa Bongo Diamond Platnumz, Esma Khan ameolewa rasmi.

Esma na mchumba wake Jembe One almaarufu Cheedy walifunga ndoa siku ya Alhamisi jioni katika hafla ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na familia na marafiki.

Miongoni mwa waliokuwepo ni mamake Diamond, Mama Dangote, dada yake Queen Darleen na binamu zao Ricardo Momo na Iddy Santos.

“Allah wewe ndiye uliyenipa huyu hakika nitamtunza na kumfunza yaliyo mema na kumkataza mabaya,” Jembe One aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram Ijumaa jioni kufuatia kukamilika kwa tukio hilo lenye mafanikio.

Aliongeza, “Hakika nakupenda sana mke wangu @_esmaplatnumz.”

Jembe One ni mfanyabiashara maarufu wa Tanzania ambaye pia ni meneja wa mwimbaji Mavokali.

Video za hafla hiyo ya Alhamisi usiku zilizoshirikishwa na Wasafi Media zilionyesha mjasiriamali huyo akiwasili kwenye ukumbi wa harusi akiwa amevalia kanzu jeupe maridadi. Ndugu za Esma wakiongozwa na Ricardo Momo na Queen Darleen kisha wanaonekana wakimzuia kuingia ndani hadi atoe kiasi fulani cha pesa.

Baada ya kutoa pesa hizo na kuruhusiwa kuingia, alienda hadi mahali alipokuwa amekaa mkewe huku akiwa amejifunika kitambaa usoni. Kisha anaonekana akimuombea kabla ya programu zingine za harusi kuendelea.

Esma na Jembe One wamekuwa wakichumbiana kwa miezi kadhaa kabla ya kufanya rasmi muungano wao Alhamisi jioni. Dada huyo kwa Diamond ana watoto wawili kutoka katika mahusiano yake ya awali.

Mwaka wa 2020, mama huyo wa watoto wawili aliolewa kama mke wa tatu na Maulid Msizwa.

Ndoa ya Esma ilidumu miezi mitatu tu baada ya sherehe ya harusi yake ya kifahari.

Miezi kadhaa iliyopita, Esma alisema kwamba amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na anatarajia kuolewa hivi karibuni.

Alimtaja mwanamume wake kama mwanaume mwenye akili zaidi kuwahi kutokea.

"Yeye ni mchapakazi na ana akili kila wakati na sura yake ni ya kufa," alisema, na kuongeza kuwa yuko tayari kutumia maisha yake yote pamoja.

"Ndoa yangu ijayo haitadumu miezi mitatu kama ile ya awali. Siwezi kuchumbiana na mtu ambaye hawezi kuniinua