Jovial afichua maelezo yasiyojulikana kuhusu baby daddy wake

Pia alionekana kuwatahadharisha wapenzi wa baadaye wa binti huyo wake.

Muhtasari

•Jovial alichapisha picha nzuri za malkia huyo mdogo kwenye Instastori zake na kuambatanisha na jumbe maalum kumhusu.

•Jovial aliendelea kufunguka upendo wake kwa bintiye na kueleza jinsi anavyonuia kumlinda kwa namna yoyote ile.

Jovial
Image: HISANI

Siku ya Jumapili, mwimbaji mashuhuri Juliet Ayub Miriam almaarufu Jovial alionyesha fahari yake kwa binti yake mdogo, Soilah.

Jovial alichapisha picha nzuri za malkia huyo mdogo kwenye Instastori zake na kuambatanisha na jumbe maalum kumhusu.

Chini ya baadhi ya picha alizochapisha, alidokeza kuhusu baadhi ya maelezo machache kuhusu baba ya bintiye asiyejulikana.

"Binti yangu wa Kimasai," aliandika chini ya picha moja.

Kwa kauli yake, mwimbaji huyo mahiri ambaye ni Mluhya alidokeza kuwa baba wa mtoto wake ametokea katika jamii ya Maasai.

"Mix ya Mluhya na Maasai," aliandika kwenye  picha nyingine.

Jovial aliendelea kufunguka upendo wake kwa bintiye na kueleza jinsi anavyonuia kumlinda kwa namna yoyote ile.

Pia alionekana kuwatahadharisha wapenzi wa baadaye wa binti huyo wake.

Miezi michache iliyopita, mwimbaji huyo wa kibao 'Jeraha' alidokeza kuhusu uhusiano mzuri kati yake na mzazi mwenzake asiyejulikana licha ya kutokuwa pamoja tena.

Katika moja ya machapisho yake ya mara kwa mara, Jovial aliweka wazi kwamba mwanaume anayetazamia kuchumbiana naye ni sharti awe na sifa zinazokaribia kufanana na za mzazi huyo mwenzake.

"Huwa nasema hivi, mwanaume yeyote ambaye atanichumbiana na mimi anapaswa kuwa angalau nusu kama baba ya mtoto wangu.. Jamani, jamaa huyo kila siku yuko nyuma yangu. Ama ni juu sina drama," aliandika.

Aidha alimtaka mwanaume huyo kuendelea kuwa mzuri kwake na binti yao kama jinsi alivyokuwa.

"Binti yangu ana baba wa kweli," alisema.

Kuna maelezo machache sana kuhusu uhusiano wa awali wa mwimbaji huyo, baba wa bintiye ni nani na kwa nini aliachana naye.