Jux ajibu madai kuwa alishindwa kumpa Vanessa Mdee ujauzito kwa kuwa hana uwezo

Muhtasari

•Jux alisema kuwa yeye pamoja na Mdee hawakuwa tayari kuwa wazazi , sio kwamba eti ako na tatizo lolote la uzazi.

•Aliweka wazi kwamba kufikia sasa  bado hajafikia kupata mtoto na mwanamke yeyote ambaye amewahi kuwa naye.

Juma Jux azungumzia madai ya tatizo la uzazi
Juma Jux azungumzia madai ya tatizo la uzazi
Image: HISANI

Nyota wa Bongo Juma Mussa Mkambala almaarufu kama Jux amepuuzilia mbali madai kwamba alishindwa kumpa ujauzito mpenzi wake wa zamani Vanessa Mdee kwa kuna hana uwezo wa kuzalisha.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Jux alieleza kwamba alikosa kupata mtoto na mpenzi wa sasa wa Rotimi kwa sababu wakati haukuwa sawa.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa yeye pamoja na Mdee hawakuwa tayari kuwa wazazi , sio kwamba eti ako na tatizo lolote la uzazi.

"Kila kitu huwa na mpango. Ule muda ambao tulikuwa pamoja ulikuwa muda ambao mimi na yeye tulikuwa hatuko tayari kuwa hivo. Kuzaa na mtu yeyote wa nje ni maamuzi, sio mabaya. Labda ilifikia muda kwenye mahusiano akawa sasa anataka. Ule muda ambao alikuwa anataka basi akawa hayuko na mimi. Mimi pia nina mipango yangu ya maisha. Siwezi kuzaa mtoto kwa sababu watu wanasema niwe na mtoto" Jux alisema. 

Jux aliweka wazi kwamba kufikia sasa  bado hajafikia kupata mtoto na mwanamke yeyote ambaye amewahi kuwa naye.

Mwanamuziki huyo alisema atapiga hatua ya kuwa mzazi wakati ambapo atajihisi yuko tayari na hatakubali kushinikizwa na watu.

"Nafanya  kitu kulingana na malengo yangu. Ikifika muda nihisi naweza kuwa na mtoto basi nitapata. Sina mtoto yeyote hadi sasa hivi lakini nitafanya kitu kulingana na muda wangu na sio kulingana na vile watu wananipangia" Jux alisema.

Alisema kwamba wakati alikuwa kweye mahusiano na Bi Mdee hawakuwahi zungumzia suala la kupata mtoto.

Jux pia alisisitiza kuwa hana kinyongo chochote dhidi ya mpenzi huyo wa zamani na kusema kwamba anamtakia mazuri katika mahusiano yake mapya.