Manzi wa Kibera aeleza kwa nini hajamuonjesha 'asali' mchumba wake mzee

Manzi wa Kibera ameweka wazi kuwa bado hajashiriki tendo la ndoa na mchumba wake mzee.

Muhtasari

•Manzi wa Kibera anaaminika kuwa kwenye mahusiano na mzee wa miaka 66 anayedaiwa kumvisha pete ya uchumba mwezi uliopita.

•Wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu, shabiki mmoja alimuuliza, "Mzee anafikisha rounds ngapi?"

Manzi wa Kibera na mchumba wake wa miaka 66
Image: INSTAGRAM// MANZI WA KIBERA

Mwanasoshalaiti Sharifa Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera ameweka wazi kuwa bado hajashiriki tendo la ndoa na mchumba wake mzee.

Manzi wa Kibera anaaminika kuwa kwenye mahusiano na mzee wa miaka 66 anayedaiwa kumvisha pete ya uchumba mwezi uliopita.

Licha ya kuchumbiana kwa muda mrefu, kipusa huyo anayezungukwa na sarakasi nyingi maishani hata hivyo amebainisha kwamba anasubiri ndoa rasmi ili kumuonjesha mchumba huyo wake zawadi ya ndoa aliyomhifadhia.

Wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu cha hivi majuzi kwenye mtandao wa Instagram, shabiki mmoja alimuuliza, "Mzee anafikisha rounds ngapi?" kumaanisha (Mzee hudumu kwa muda gani kitandani)

Manzi wa Kibera bila kusita alijibu, "Mpaka tufunge ndoa ndio tutafanya tendo hilo."

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya mrembo huyo kutoka mtaa wa Kibera kudaiwa kuvishwa pete ya uchumba na mzee huyo.

Katika video zilizovuma kwenye mitandao ya kijamii, mwanasosholaiti huyo asiyepungukiwa na drama alionekana akiwa ameandamana na mchumba wake kabla ya mzee huyo kupiga magoti na kumuomba wafunge ndoa. Makumi ya watazamaji kisha walisikika wakimtia moyo kukubali ombi hilo la ndoa.

"Sawa, nishasema ndio!" alisikika akimwambia mpenzi huyo wake baada ya muda mfupi wa kufikiria na kuzingatia.

Baada ya kukubali, mzee huyo aliyekuwa amevalia kapura nyeupe na koti nyeusi alionekana akimvisha pete ya uchumba.

Watazamaji waliweza kusikika wakimsihi mwanasosholaiti huyo kumbusu mchumba wake na  wanaonekana kutii ombi.

"Kama unapenda, weka pete kwenye kidole," mwanasoshalaiti huyo alisema kwenye Instagram baada ya tukio hilo.

Katika video aliyochapisha pamoja na ujumbe huo, alionekana akijigamba kuhusu mpenzi wake na pete aliyomvisha kidoleni.

Baadaye, mwanasosholaiti huyo alidokeza kufunga pingu za maisha na mchumba huyo wake katika siku za hivi karibuni.

Katika tangazo lake mwezi uliopita, alikejeli harusi ya mwimbaji Akothee ya hivi majuzi na kudokeza kuwa yake itakuwa kubwa zaidi.

"Harusi yangu itakuwa kubwa kuliko ucheshi huu," aliandika kwenye picha ya Akothee na mumewe siku ya harusi yao.