Mwanadada amshutumu Zari Hassan kwa kuiba mume wake Shakib, atoa cheti cha ndoa

Nalule na Shakib walifunga ndoa Juni 2016.

Muhtasari

•Mimi ameibua madai kuwa yeye ndiye mke halali wa Bw Lutaaya na hata kutoa cheti cha ndoa kuthibitisha madai yake.

•Mimi anamshtumu Shakib kwa kuikimbia ndoa iliyofungwa kisheria ili kuwa na Zari ambaye ni maarufu na tajiri zaidi.

Zari Hassan, Shakib Cham, Mimi Nalule
Image: HISANI

Mwanamke mmoja wa Uganda anayeishi Marekani amejitokeza kumshutumu mwanasosholaiti Zari Hassan kwa 'kumuibia' mume wake Shakib Cham Lutaaya.

Nalule Shamirah Sembatya almaarufu Mimi ameibua madai kuwa yeye ndiye mke halali wa Bw Lutaaya na hata kutoa cheti cha ndoa kuthibitisha madai yake.

Kulingana na cheti ambacho ameonyesha,inaonekana wawili hao walifunga ndoa mwezi Juni 2016 baada ya kuchumbiana kwa muda.

Mimi pia anadai kwamba mnamo Mei 2017 alimpa Shakib visa ya Amerika kama mchumba wake, hivyo kumpa uwezo wa manufaa kadhaa.

Kipusa huyo sasa anamshtumu mpenziwe Zari kwa kuikimbia ndoa iliyofungwa kisheria ili kuwa na Zari ambaye ni maarufu na tajiri zaidi.

Cheti cha ndoa cha Mimi na Shakib
Image: HISANI

Hivi majuzi Zari alifichua kuwa tayari amepiga hatua ya kukutana na wazazi wa mpenzi wake Shakib Lutaaya na kubainisha kuwa yuko tayari kupeleka mahusiano yao ya miezi kadhaa katika kiwango cha juu zaidi.

"Shakib alinipeleka kuwaona wazazi wake na ilikuwa nzuri sana," Zari alisema.

Mahusiano ya Zari Hassan na Shakib yamekuwa yakikosolewa sana hasa kwenye mitandao ya kijamii suala kuu likiwa tofuati zao za umri. Zari ana umri wa miaka 42 ilhali mpenziwe alitimiza miaka 31 hivi majuzi.

Mama huyo wa watoto watano hata hivyo alibainisha kuwa wazazi wa Shakib hawakuashiria tatizo lolote na mahusiano yao na kubainisha kuwa mkutano wao ulikuwa mzuri.

“Alinipeleka kuonana na wazazi wake na walikuwa wazuri sana, na sikumbuki hata kidogo wakilalamika kuhusu uhusiano huo,” mzaliwa huyo wa Uganda alisema na kuongeza kuwa hatajitetea kabisa.

Zari pia alifichua kuwa anapanga kuongeza watoto zaidi na Shakib lakini akabainisha kuwa si kwa sababu ya shinikizo la umma.