"Raha ya mahusiano ni kufanyiana ujinga!" Diamond atoa ushauri muhimu wa mahusiano

Diamond alibainisha kuwa mzaha kidogo husisimua mahusiano.

Muhtasari

•Diamond amewashauri wanandoa kutokuwa serious sana katika jinsi wanavyohusiana kila wanapokuwa pamoja.

•Pia aliwataka kutosikiliza ushauri mwingi kutoka kwa watu ambao hawahusiki kamwe katika mahusiano yao.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa Bongo Diamond Platnumz amewashauri wanandoa kutokuwa serious sana katika jinsi wanavyohusiana kila wanapokuwa pamoja.

Wakati akiwahutubia mashabiki wake katika tamasha la Cheers 2023, Diamond aliwabainishia kuwa mzaha kidogo husisimua mahusiano.

"Kwenye mahusiano wakati mwingine, raha ya mahusiano ni kufanyiana ujinga. Ukiambiwa baby lala unalala, baby amka unaamka, baby usiende kazini usiende kazini," Diamond aliwaambia mashabiki kabla ya kucheza wimbo wake 'Ukimuona.'

Bosi huyo wa WCB aliwaonya wapenzi dhidi ya kuruhusu watu wengine kuingilia mahusiano yao na kuharibu kitu kizuri walichojenga pamoja.

Pia aliwataka kutosikiliza ushauri mwingi kutoka kwa watu ambao hawahusiki kamwe katika mahusiano yao.

"Mambo ya watu wawili ndani msitake watu wengine waingilie. Ushauri mwingi sana tuwache jamani," alisema.

Baba huyo wa watoto wanne aliendelea kuwakosoa marafiki wabaya wanaoharibu mahusiano kupitia wimbo wake wa Ukimuona.

Haya yanajiri huku staa huyo wa Bongo akidaiwa kuwa kwenye mahusiano na msanii wake Zuchu. Wawili hao ambao nyota yao ya kimuziki imeendelea kung'aa wamekuwa wakidaiwa kutoka kimapenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mwezi uliopita hata hivyo, Diamond alijitokeza wazi na kukana kuchumbiana na Zuchu licha ya  wawili hao kunyoosha maelezo kuwa ni wapenzi hapo awali.

Diamond katika wimbo wake mpya wa Chitaki, kuna vesi moja ambayo anasikika akisema kuwa wanaosema anachumbiana na Zuchu ni wazushi tu ambao wanatafuta sababu ya kuendelea kumsema yeye na msanii huyo wake.

“Wewe ndio mwisho wa reli, kwako naweka nukta. Waliokuambia natoka na Zuchu si kweli wanazusha. Wao ndio kazi yao sisi kutuhukumu…”  anasikika akiimba.

Hapo awali Diamond aliwahi kuwa kwenye mahusiano yasiyofanikiwa na mwanasoshalaiti wa Uganda Zari Hassan, mwimbaji wa Kenya Tanasha Donna, mwanamitindo Hamisa Mobetto, muigizaji Wema Sepetu, Irene Uwouya, Rehema Fabian, Tunda Sebastian miongoni mwa wanawake wengine.