Siasa, Ndoa, Kanisa..: Terence aorodhesha mambo 10 ambayo anadai Kibe ameshindwa

Terence alimtaja mtumbuizaji huyo kama mtu aliyeshindwa maishani.

Muhtasari

•Kibe alimkosoa na kumkejeli mchekeshaji huyo kufuatia video yake akicheza densi ambayo alikuwa amechapisha.

•Mchekeshaji huyo alimtaka Kibe kujitokeza kukosoa jambo lolote alilosema uwongo katika taarifa yake.

Terence Creative na Andrew Kibe
Image: HISANI

Mchekeshaji Lawrence Macharia almaarufu Terence Creative amejibu ukosoaji wa mwanapodcast Andrew Kibe.

Hivi majuzi, Kibe alimkosoa na kumkejeli mchekeshaji huyo kufuatia video yake akicheza densi ambayo alikuwa amechapisha.

Katika jibu lake siku ya Jumamosi asubuhi, Terence alimtaja mtumbuizaji huyo kama mtu aliyeshindwa maishani.

"Ninapenda sanaa, kama msanii naweza kuwa chochote na mhusika yeyote, naishi kwa ajili ya sanaa na hilo halitabadilika, angalau hiyo imenifanyia kazi tofauti na ile failure inaitwa kibe," alisema kwenye Tiktok.

Mchekeshaji huyo aliendelea kuandika orodha ya mambo kumi ambayo alidai Kibe amewahi kushindwa kufikia sasa.

"1. Akaanzisha duka la  kuuza CDs inaitwa Media kali ikafeli

2. Akakuwa Mhubiri pale Langata Family Gospel ikafeli juu ya kula kondoo.

3. Akajaribu kuwa mbunge wa Lang’ata akafail.

4. Akasema Jalas hatapata kiti cha Mp,jalas akapata Kibe akafeli.

5.Kibe akajaribu ndoa,akawa mwenye sumu na mwenye kujipenda akashindwa kushughulikia familia bibi na watoto wakatoroka akafeli," aliandika Terence.

Aliendelea;

6.inadaiwa Kibe akashindwa kuchumbiana na watu wa rika yake akaanza na wenye umri mdogo akashikwa akatoroka kenya akaenda marekani.

7. Amerika ameshindwa na kazi sasa anawekwa na masharti ni kwamba hafai kuonyesha mahali anakaa isipokuwa hiyo kona ya makofia lakini tunajua.

8. Baada ya kuanguka langata mp akajaribu kuanzisha Biker Gang akafeli.

9. Kibe akaanza Radio hakuperform akafutwa

10. Saa hii anajaribu Youtube lakini but mwishowe"

Mchekeshaji huyo mahiri alimtaka Kibe kujitokeza kukosoa jambo lolote alilosema uwongo katika taarifa yake.

Siku chache zilizopita, Kibe katika mojawapo ya vipindi vyake, alidai kwamba mchekeshaji huyo amekaliwa.

Alichapisha video ya Terence akicheza dansi za ajabu huku akiwa amevalia kaptura na kutupilia mbali kile ambacho alikuwa akifanya kuwa uchekeshaji huku akidai kwamba ni tendo la kudhalilisha mwanamume