"Vidonda vingine haviponi!" Amira azidiwa na hisia baada ya mumewe Jimal Rohosafi kuomba msamaha

Amira ameomba neema ya Mungu anapoendelea kutafakari suala hilo

Muhtasari

•Amira amesema kwa sasa hawezi kuuelewa msamaha wa mumewe  kwani umefufua kumbukumbu ya siku mbaya za nyuma.

•Amira ameomba neema ya Mungu anapoendelea kutafakari suala hilo na kueleza kuwa kwa sasa amezidiwa na hisia.

Image: INSTAGRAM// BEING AMIRA, JIMAL MARLOW ROHOSAFI

Mfanyibiashara Amira hatimaye ametoa jibu lililokuwa limesubiriwa kwa hamu kwa barua la mumewe la kuomba msamaha.

Jumamosi mwenyekiti wa muungano wa wamiliki matatu jijini Nairobi, Jimal Rohosafi, alichapisha  akimuomba radhi mama huyo wa watoto wake wawili kwa drama nyingi alizosababisha kwenye ndoa yao mwaka jana.

Tangu Jimal achukue hatua hiyo wanamitandao wamekuwa na hamu kubwa ya kuona majibu ya Amira kwani Jumapili aliahidi kulihutubia taifa baada ya kurejea nchini kutoka Tanzania.

"Wacha nirudi ndo ni address the nation nikiwa homeground!" Amira aliandika Jumapili kwenye Instastori zake.

Hatimaye mfanyibiashara huyo aliweza kurudi nchini na kufuatia shinikizp kubwa la wanamitandao sasa amedondosha jibu lake.

Amira amesema kwa sasa hawezi kuuelewa msamaha wa mumewe kwani umefufua kumbukumbu ya siku mbaya za nyuma.

"Ombi hilo la msamaha limenirudisha katika sehemu moja ya giza ambayo nimewahi kuwa katika maisha yangu kwa sababu nimetafakari juu ya mengi yaliyotokea hadharani na nyuma ya milango iliyofungwa na imezua hisia nyingi," Amira alijibu kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto wawili ameomba neema ya Mungu anapoendelea kutafakari suala hilo na kueleza kuwa kwa sasa amezidiwa na hisia.

"Vidonda vingine haviponi, lazima ujifunze jinsi ya kuishi navyo," Aliandika.

Katika ombi lake la msamaha Jimal alikiri kuwa alimkosea sana mkewe kwa kutekeleza wajibu wake wa kumlinda.

Alimuomba mkewe apokee ombi lake la msamaha huku akimkumbusha jinsi ambavyo wamepitia mengi pamoja.

"Ilikuwa mbaya kabisa. Huenda nilionekana kama mtu asiye na wasiwasi lakini sikuwa na la kufanya. Nilijua haikuwa sawa, nilijua unaumia lakini sikuweza kujikusanya!Amira nafanya hivi kwa sababu ukosefu wa heshima pia ulikuwa mkubwa. Naomba radhi kwa kukosa heshima," Aliandika.

Mwenyekiti huyo wa muungano wa wamiliki matatu pia alifichua kwamba hajakuwa sawa tangu alipokosana na mke huyo wake.

Alidokeza kuwa yupo tayari kupiga hatua zozote ili kufufua ndoa yao iliyokufa miezi kadhaa iliyopita.

Mwaka jana ndoa ya Jimal iliindia doa baada yake kujitosa kwenye mahusiano na mwanasoshalaiti Amber Ray.

Jimal alimchukua Amber Ray kama mke wake wa pili, hatua ambayo ilisababisha drama zisizoisha kwenye ndoa yake.

Mfanyibiashara huyo alikumbwa na mkanganyiko kuhusu amchague nani wakati wake wake wawili walipoanza kuzozana..

Baadae aliamua kumchagua Amber Ray, jambo ambalo lilimkera Amira ambaye mwezi Novemba alianza mikakati ya talaka.