Whozu afunguka kuharibika kwa mimba ya Wema Sepetu, aapa kumpa ujauzito mara nyingine

Mwimbaji huyo amethibitisha kuwa alimpachika mimba Wema Sepetu ila ikaharibika.

Muhtasari

•Whozu alieleza kusikitishwa kwake na watu waliotilia shaka habari za yeye kumpachika mimba mpenziwe.

•Whozu alisema kuwa  yeye na mpenziwe wanatamani kupata mtoto wa kiume pamoja.

Whozu na Sepetu

Mwimbaji wa Bongo Whozu amethibitisha kuwa ni kweli alimpachika mimba mpenzi wake Wema Sepetu ila ikaharibika.

Katika mahojiano na waandishi wa habari, Whozu alibainisha kuwa kuharibika kwa ujauzito wa Wema ilikuwa  bahati mbaya.

Mwanamuziki huyo alieleza kusikitishwa kwake na watu waliotilia shaka habari za yeye kumpachika mimba mpenziwe.

"Iliniuma. Alafu watu wanafikiria ni uwongo! Mnanionaje kuwa mimi siwezi kumpa mtu mimba? Mnanichukuliaje?,"  alisema.

Alidokeza kuwa anapanga kumpachika Wema ujauzito kwa mara nyingine baada ya ule wa kwanza kutofikia hatua ya kujifungua.

Whozu alisema kuwa  yeye na mpenziwe wanatamani kupata mtoto wa kiume pamoja.

"Lazima niweke pale. Lazima kuwa na Lola na mdogo wake Lola. Naomba Mungu awe wa kiume. Mamake atakuwa Wema Sepetu," alisema.

Mwimbaji huyo alisema kuwa bado anafanya juhudi nyingi na pia anamuombea sana mpenzi wake apate ujauzito tena.

Haya yalijiri baada ya Wema Sepetu kueleza hamu yake ya kupata mtoto wa kwake na kumuomba Mungu amjalie.

Ijumaa, aliandika ombi la mtoto chini ya picha yake akiwa amemshika mtoto mchanga ambayo alipakia kwenye Instagram.

"Eh Mungu tafadhali nibariki na wangu siku moja🙏🙏🙏," alisema.

Wema alikiri kuwa kumtazama mtoto huyo mchanga mikononi mwake kulimfanya ajisikie kuwa kuenda naye awe wake.

"Nilitamani nikimbie naye wallahy🥺🥺🥺" alisema.

Chini ya chapisho hilo, Whozu alimtambua muigizaji huyo kama Mama K.

Siku ya Jumamosi, Wema alimmiminia sifa mpenzi huyo wake na kumtambua kama baba ya mtoto wake wa siku za usoni.

"Amore, Chibaba, Mpenzi wa maisha yangu, Baby Daddy wa siku za usoni, furaha, nambari moja, mapenzi yasiyo na mwisho @whozu," aliandika chini ya video ya Whozu ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hadi wa leo, Wema Sepetu ambaye ana umri wa miaka 32 bado hajaweza kumshika mtoto kutoka tumboni mwake.

Kwa miaka mingi, muigazaji huyo amekuwa akishambuliwa na kukejeliwa mitandaoni kutokana na hali yake. Wengine hata hivyo wamekuwa wakimfariji na kumtia moyo mpenzi huyo wa zamani wa Diamond.

Takriban miaka minne iliyopita Wema aliwahi kufunguka kuhusu  tatizo kwenye tumbo lake la uzazi linalomzuia kushika ujauzito.

“Unajua mimi nilikuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa tumbo langu la uzazi lililosababisha nisiweze kuzaa kwa muda wote huu. Ngoja niweke wazi leo watu wajue, mimi nina ugonjwa ambao unasababisha mayai yangu ya uzazi kutoboka na kushindwa kupevusha mbegu za uzazi," Alisema katika mahojiano na Global Publishers.