Wema Sepetu: Mimi sijui, naona kidogo ndoa hapana, siko tayari kuolewa na Whozu

Whozu na Sepetu wamekuwa kwenye mahusiano kwa wiki chache zilizopita huku wakiitana majina ya majazi Chibaba na Chimama.

Muhtasari

• Wengi wanasema anajidhalilisha kuingia katika uhusiano na Whozu ambaye wengi walimtaja kama mdogo si tu kiumri bali pia kiumaarufu.

Sepetu akana kuolewa na Whozu
Sepetu akana kuolewa na Whozu
Image: Instagram

Mwigizaji mkongwe katika filamu za Bongo, Wema Sepetu ametema ya moyoni kuhusu uhusiano wake na msanii Whozu.

Akizungumzia kupitia kipindi chake cha My Truth ambacho anakipakia kweney program yake ya Wema, pia alipakia kionjo cha mzungumzo hayo kwenye Instagram yake na kuweka wazi kwamba hayupo tayari hata kidogo kuingia katika ndoa na mpenzi huyo wa zamani wa msanii Tunda – Whozu.

Kama ambavyo jina la kipindi hicho chake linakwenda, Sepetu alizungumza fikira zake na ukweli wake kwamba hayupo tayari kabisa kuolewa na Whozu, na kuwaacha wengi wakijiuliza iwapo uhusiano wake na kijana huyo wa watu bado upo imara au ndio mwanzo nyufa zimeanza kujitokeza.

“Mimi sijui, naona kidogo ndoa… ndoa yaani siko tayari kuolewa na Whozu,” Sepetu alisema kwa kudokeza huku klipu hiyo ikikatika.

Itakumbukwa Wema Sepetu na msanii Whozu walianza uhusiano wao takribani mwezi mmoja uliopita na wamekuwa wakipigwa vita mitandaoni ambapo wengi wanasema anajidhalilisha kuingia katika uhusiano na Whozu ambaye wengi walimtaja kama mdogo si tu kiumri bali pia kiumaarufu.

Wiki mbili zilizopita, Whozu alimpeleka Sepetu kisiwani Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo walipakia picha za kutmanisha wakijivinjari na kula bata aliyenona.

Inashangaza leo hii Sepetu akidokeza kwamba uhusiano wake na Whozu si wa muda mrefu na katu hautakuja kudumu, katika kile amabcho anadokeza kwamab bado atalazimika kurudi sokoni ili kumtafuta mwanaume wa ndoto zake.