Whozu amrushia mpenzi wake Sepetu tafrija ya kukata na shoka Zanzibar

Mwanamuziki Whozu alimpeleka Wema Sepetu Zanzibar kusherehekea siku ya kuzaliwa

Muhtasari

• Sepetu alimshukuru mpenzi wake kwa mtoko huo na pia kwa sherehe yake ya kushtukiza na kuwa alijihisi kama mwanamke aliye barikiwa.

Image: INSTAGRAM// WEMA SEPETU

Mwanamuziki Whozu alimpeleka Wema Sepetu Zanzibar kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwigizaji huyo wa Bongo.

Wapenzi hao walijivinjari kwenye mtoko huo huko Zanzibar kwa siku tatu ambapo walijiburudisha kwa kusherehekea .

Sepetu na Whozu waliishi kwenye hoteli kwa siku hizo tatu na kujitumbuiza na kusherehekea kulingana na machapisho  ya wapenzi hao wawili ya Instagram.

Mwigizaji huyo alisema kuwa Whozu aliyatilia maneno yake maanani kwa kumpeleka kwenye mtoko huo na kuwa alihakikisha wamekamilisha siku tatu.

"Niliambiwa na Chibaba kuwa birthday inaisha Jumatatu. Na kweli bwana, imeisha leo. Chibaba kahakikisha maneno hayaendi chini. Naweza sema mwaka huu umekuwa miongoni mwa miaka bora zaidi. Kubarikiwa na mwaka mwengine, kubarikiwa na furaha, kubarikiwa na upendo," alisema.

Sepetu alimshukuru mpenzi wake kwa mtoko huo na pia kwa sherehe yake ya kushtukiza na kuwa alijihisi kama mwanamke aliye barikiwa na bahati kwa wote.

"Kwako wewe Chibaba wangu. Asante kwa kila kitu. Unaweza kuona hiki ni kidogo bali hujui tu kina ukubwa gani kwangu na jinsi gani umegusa moyo wangu. Ningepnda ujue jinsi ulivyonifurahisha . Nitaendelea kukuombea kwa Mungu ili akubariki kwa sababu unastahili kila jema maishani mwako. Nakupenda na asante," alisema Sepetu akiwa na furaha.

Sepetu alisema kuwa hakuwa amepanga chochote kwa siku yake ya kuzaliwa ila marafiki wake na wanaompenda akiwemo Whozu hawakukubali siku hiyo ipite bila kumfanyia chochote.

Mwigizaji huyo hakuwa na mpango wa kupigwa picha ili ziwe kumbukumbu za hiyo siku na alikuwa amepanga kumaliza siku hiyo kama siku nyingine yoyote.

Alisema kuwa alikuwa amepanga kuingia Instagram live ili kuwatumbuiza mashabiki wake ila akapata ujumbe kuwa mama yake anakuja kutoka Moshi na angetaka kumwona kwa siku hiyo .

Sepetu alisema kuwa hakuwa anatarajia alichokipata alipoenda kumwona 'mama yake' na kuwa alijiona mtu maalum na anayependwa.

Mwigizaji huyo alipata ameandaliwa sherehe ya kushtukiza ya siku yake na Whozu ambaye alipanga na rafiki zake ili kumsherehekea mwigizaji huyo ambaye hakuwa amepanga lolote siku hiyo.

"Nilijiona special sana nisiwe muongo, nikaona dunia yote yangu. Mpaka dakika hii bado nahisi hivyo. Nyie, nyie,mh. Kupendwa raha," alisema.

Aliwashukuru mashabiki wake kwa kumwonyesha upendo zaidi ya yote siku hiyo .

Hii ni baada ya Sepetu kumtambulisha mwanamuziki huyo kama mpenzi wake siku chache kabla ya siku hiyo ya kuzaliwa kwake.