Willis Raburu atumia 900,000 kupunguza uzito wa mwili

Mtumbuizaji huyo alisema ilichukua siku tatu kwake kufanyiwa upusuaji.

Muhtasari

•Mtumbuizaji Willis Raburu amesema alifanyiwa upasuaji wa tumbo uliogharimu kati ya  laki Ksh 600 na Ksh 900.

•Alisema alichagua kufanyiwa upasuaji huo kwa kuwa kufanya mazoezi kwenye gym hakukumsaidia kupunguza uzito.

Mtangazaji Willis Raburu katika muonekano mpya bila rasta
Mtangazaji Willis Raburu katika muonekano mpya bila rasta
Image: Willis Raburu//Facebook

Mtumbuizaji Willis Raburu amefichua kwamba alilazimika kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito kwa ajili ya afya yake.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Raburu alisema alifanyiwa upasuaji wa tumbo uliogharimu kati ya  laki Ksh 600 na Ksh 900.

Aliongeza kuwa alichagua kufanyiwa upasuaji huo kwa kuwa kufanya mazoezi kwenye gym hakukumsaidia kupunguza uzito.

“Nilienda kufanyiwa gastric bypass surgery, naheshimu watu wanaenda gym, Gym ni kazi, nilikua na wakufunzi wazuri lakini nilikua napunguza uzito na baada ya muda mfupi  unarudi'' Raburu alisema.

"Wakati nilienda kufanyiwa upasuaji sikuwa nahisi vizuri. Nilikuwa na kilo 164 nilihitaji upasuaji kwa sababu shinikizo la damu na cholesterol ilikuwa juu," aliongeza.

Willis alisema ilichukua siku tatu kwake kufanyiwa upusuaji katika hospitali ya Nairobi Biatric, na baada ya hapo ilimchukua muda kupona.

Aliongeza kuwa daktari alipendekeza akule chakula kilichopondwa kwa muda wa wiki nne, kwa kuwa tumbo yake haikuwa na uwezo wa kubeba uzito fulani wa chakula baada ya upasuaji.

Mtangazaji huyu pia alidokeza kuwa alianza kuona mafanikio baada ya mwezi moja,

''Nilipunguza kilo kutoka 164 hadi 150, ukiona ata picha zangu zenye nilipiga nikiwa na kilo 164, na venye unaniona sai, najua kuna tofauti kubwa sana' Raburu alisema.

Aidha, alibainisha kuwa mtu anapoongeza kilo zaidi kupita kiasi, lazima akuwe na wasi wasi, yeye mwenyewe alikuwa na hofu kuhusu afya yake.

''Si vizuri kuamka asubuhi, na ukijaribu kuvaa nguo zako unakuta kwamba hazikutoshi, Kuna wale ambao wanajawa na furaha wanapoongeza kilo, na kuna wale ambao hawafurahishwi kuwa na mwili kubwa, mimi ni mmoja wao, kwa hivyo lazima ningetafuta usaidizi wa haraka wa kiafya'' Raburu alisema.

Alisema yeyote ambaye angependa kufanyiwa upasuaji, lazima afanye maamuzi makubwa kwanza.

"Ukiona kuwa kufanya zoezi inaweza kukusaidia kupunguza kilo, basi enda zoezi usijilazimishe kuenda upasuaji."