(+video) DJ Bash azua drama katika klabu moja Nairobi akidai malipo yake

Mcheza santuri huyo alifika klabuni hapo saa nane asubuhi akiteta vikali kutolipwa.

Muhtasari

• Baadae kwenye ukurasa wake wa Instagram, mcheza santuri huyo alisema kwamba mgogoro ule ulipata suluhu na hata kushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kumpa haki yake.

Mcheza santuri maarufu nchini Kenya DJ Bash katika moja ya video zinasozungumziwa sana mitandsoni alionekana akizushiana kwa cheche kali na walinzi katika sehemu moja ya burudani jijini Nairobi alikoenda kudai malipo yake baada ya kutumbuiza klabuni humo.

Kwenye video hiyo, Bash anaonekana akiingia kwacfujo klabuni hapo huku akijaribu kuzuiwa na walinzi ila anasisitiza kutaka kuingia ili kuzungumza na mwenye klabu kumpa malimbikizi yake aliyokuwa akidai kwamba baada ya kuburudisha wanywaji hakupatiwa kilichochake kama maafikiano ya awali.

Video hiyo saa kadhaa baadae ilifutwa ila kuna baadhi ya watu waliofanikiwa kuipakua hata kabla ya mwenye kuipakia kuidungua na Bash anaonekana akiletana juu na walinzi huku akisema anataka kuingia ili kuchukua mashine ya santuri kama ridhaa ya malipo yake aliyokuwa akiwadai wenye klabu hiyo.

Bash alifanikiwa kufikia kaunta ya deejaying ya klabu lakini hakupata kitu chenye thamani ya pesa zake. Kikosi cha usalama kilijaribu kumzuia lakini hakukata tamaa. Hatimaye walifanikiwa kumpigia simu mmoja wa wasimamizi ambaye alimtuliza huku akiahidi kufanya malipo siku iliyofuata.

Katika mojqa ya maongezi yake na walinzi hao, Bash anasikika akisema kwamba nis aa nane asubuhi ambapo alikuwa amefika pale kudai pesa zake na kupata watu wengi wameondoka sehemu hiyo na kuelekea makwao huku himaya hiyo ikiwa imebaki chini ya walinzi pekee na kiza totoro cha kuukaribisha mwanga wa alfajiri.

Baadae kwenye ukurasa wake wa Instagram, mcheza santuri huyo alisema kwamba mgogoro ule ulipata suluhu na hata kushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kumpa haki yake.