Willy Paul asifia umbo na urembo wa mwanasoshalaiti Amber Ray

Muhtasari

• Msanii Willy Paul amepelekea katika mitandao ya kijamii kusifia urembo wa mwanasosholaiti Amberay.

• "Hiyo nguo imepiga kona, chochote unachoona kwake ni real," aliandika.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Willy Paul

Msanii Willy Paul amezamia kwenye ukurasa wake wa Instagram kusifia urembo wa mwanasosholaiti Amberay.

Kupitia ujumbe aliochapisha Jumanne, Pozze alisema kwamba Amberay ni mwanamke 'natural' ambaye hafanyi chochote kufurahisha umma.

Willy Paul alisema kwamba Amberay ana figa nzuri ambayo imewaacha wengi wakidata. Ameongeza kuwa Amber hajafanya upasuaji wowote kuongeza sehemu za mwili wake.

"Hiyo nguo imepiga kona, chochote unachoona kwake ni real," aliandika.

Kauli ya Willy Paul inajiri siku chache baada ya kushuhudiwa mkwaruzano kati ya Amberay na Nicah the Queen  kuhusu urembo wao, huku Amberay akishikilia kwamba atazidi kufanya chochote kuhakikisha ngozi yake inazidi kuwa laini.

Kipindi cha nyuma kidogo, Amberay alijitokeza na kuwaambia kina dada kufanya chochote hata kama ni kuuza uchi wao maadamu wapate hela, huku baadhi wakikubaliana naye na wengine kuipinga kauli yake.

Ifahamike kwamba kumekuwa na duru za chini kwa chini kwamba Willy Paul ana mahusiano ya kimapenzi na mwanasosholaiti huyo, ila Amberay alijitokeza na kusema kwamba ana mpenzi na hata kuonekana katika hafla kadhaa wakiwa pamoja.