'Tukutane kwa bar' Iyanii atoa kibao cha Valentines

Muhtasari

•Msanii Iyanii ametoa kibao kipya ambacho kinajikita kwenye siku ya wapendanao ambacho  kinachojulikana kama ‘Tukutane kwa Bar.

•Iyanii ambaye ni msanii anayeibukia kwenye sanaa ya muziki  mwaka jana alitoa  kibao cha Pombe,ambacho kilichezwa kwenye tamasha mbalimbali za burudani.

Iyanii
Iyanii
Image: Hisani

Msanii Iyanii ametoa kibao kipya 'TTukutane kwa Bar' ambacho kinazungumzia siku ya wapendanao.

Iyanii ambaye ni msanii anayeibukia kwenye sanaa ya muziki  mwaka jana alitoa  kibao cha Pombe,ambacho kilitesa sana katika maeneo mbalimbali ya burudani.

‘Pombe’  ni mojawapo  ya vibao vya Iyanii ambavyo vilitokea kupendwa sana na wakenya hasa katika  msimu wa Krismasi.

Miongoni mwa vibao ambavyo msanii huyo ametoa na zinafanya vizuri ni  kama; Furaha na Pombe na cha hivi majuzi tukutane kwa bar.

This is to appreciate all my fans this Valentines, let me put a smile on your face as we wait for new music. Happy Valentines in advance. Written and performed by Iyanii Produced, mixed and mastered by Alexis on the beat. Additional Vocals: Princess Malikha Kiana, Iyanii, Brenan Rashid, Benson Amadi, Wilfred Waswa, Eugene Omondi, Tony Opany. Guitar: Iyanii Executive Producer: Utembe World All Rights Reserved © UtembeWorld2022

‘Tukutane kwa bar’ ni kibao ambacho kinazungumzia wale watu hawana wapenzi hasa mwezi huu wa mapenzi, anawashauri badala ya kujililia kwenye vitanda vyao wajitokeze kwenye virabu  wapige sherehe pamoja kuepusha upweke unaokumba mtu wakati hana mpenzi.

Lengo la wimbo huo ni kuleta mashabiki pamoja na kusherekea siku hio muhimu kwa wapendao na kufanya wengi kuwa na tabasamu nyusoni badala  ya kukaa kwenye kitanda usiku upweke ukiwa kumba si haba.