Erick Omondi asema vyombo vya habari vimepoteza maana.

Muhtasari

• Mcheshi kutoka Kenya Erick Omondi amefunguka na kusema kwamba vyombo vya habari humu nchini vimepoteza ushawishi wao kwa umma.

• Kulingana na ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi amesema kwamba utandawazi na utumiaji wa simu umechukua nafasi ya vyombo vya habari na kwamba katika siku zijazo watu wengi watatengeneza mamilioni ya pesa kupitia mitandao ya kijamii kama vile: YouTube, Instagram na Facebook.

erick omondi
erick omondi
Image: Hisani
erick omondi
erick omondi
Image: Hisani

Mcheshi kutoka Kenya Erick Omondi amefunguka na kusema kwamba vyombo vya habari humu nchini vimepoteza ushawishi wao kwa umma.

Kulingana na ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi amesema kwamba utandawazi na utumiaji wa simu umechukua nafasi ya vyombo vya habari na kwamba katika siku zijazo watu wengi watatengeneza mamilioni ya pesa kupitia mitandao ya kijamii kama vile: YouTube, Instagram na Facebook.

I have not been on TV since 2011 and I have managed to remain the MOST RELEVANT ARTIST in Kenya. Also the most followed,” alisema Erick Omondi.

Aidha Erick Omondi amedokeza kwamba asilimia 95 ya wakenya hawatazami taarifa na vipindi katika redio na televisheni mbalimbali humu nchini hilo likionyesha kwamba vituo hivyo vya habari vimepoteza umuhimu wake katika taifa hili.

Akitoa mfano hai, mcheshi huyo amesema kwamba hajafanya kipindi chochote katika vyombo vya habari tangia mwaka wa 2011 ila bado anasalia kuwa msanii maarufu zaidi nchini na mwenye mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo baadahi ya wanahabari hawajakubaliana naye huku wakionyesha kugadhabishwa kwao kuhusu kauli ya Omondi. Wengi wamesema kwamba vyombo hivyo vya habari ndivyo vilimsaidia kujenga jina lake na hivyo basi anapaswa kutoa heshima na sio kukashifu sehemu ambayo wakati mmoja aliitegemea kuendeleza maisha yake, na kwamba majukwaa yote yana umuhimu wake kwa umma.

Akionekana kuwa mwenye msimamo dhabiti, Erick Omondi amesisitiza kwamba katika mwaka mmoja ujao, mabadiliko katika sekta hiyo yatakuwa makubwa na kwa hivyo watu wanapaswa kujipanga vilivyo.

 

.