Harmonize na Jane Misso kwenye kibao cha injili, itakuwaje?

Muhtasari

• Msanii na mkurugenzi mkuu wa Kondegang, Harmonize anatarajiwa kuachia ngoma ya injili Jumatatu tarehe 7/02/2022.

• Hiki kitakuwa kibao cha kwanza kabisa cha injili kutoka kwa Harmonize tangu anaanza safari yake katika muziki, huku mashabiki wengi wakizidi kukuna vichwa vyao kuhusu sababu kuku iliyomlazimu ‘jeshi’ kuachia ngoma ya kumsifu Mungu.

Msanii na mkurugenzi mkuu wa Kondegang, Harmonize anatarajiwa kuachia ngoma ya injili Jumatatu tarehe 7/02/2022.

Hiki kitakuwa kibao cha kwanza kabisa cha injili kutoka kwa Harmonize tangu anaanza safari yake katika muziki, huku mashabiki wengi wakizidi kukuna vichwa vyao kuhusu sababu kuku iliyomlazimu ‘jeshi’ kuachia ngoma ya kumsifu Mungu.

Ngoma hii ambayo  atamshirikisha msanii wa injili kutoka Tanzania, Jane Misso inatarajiwa kupokelewa kwa ukubwa ikifahamika kwamba Misso amedumu katika sekta hiyo kwa muda mrefu sasa.

Kupitia video ambayo Harmonize aliachia katika ukurasa wake wa Instagram, Misso anaonekana kumuombea Kondeboy na kumpa baraka kabla yao kuachia kibao hicho.

Mashabiki kwa sasa wanasubiri kwa hamu kuona Harmoize atakavyotamba kwenye kibao hicho kwa kuwa hajawahi kuhusika tena katika ngoma za injili.

Harmonize ni moja kati ya wasanii ambao wanazidi kufanya vizuri katika muziki ndani ya bongo na Afrika mashariki kwa ujumla, huku mashabiki wakizidi kufurahia vibao vyake kila mara anapoingia studioni na kuachia kazi.