- Harmonize akanusha madai ya kutuma watu kwa mahasimu wake
Mwanamuziki wa Tanzania Harmonize amejitokeza wazi na kueleza hajawai tuma watu kuzungumza vibaya kuhusu washindani wake.
Harmonize almaarufu Konde amefunguka haya kwenye kituo kimoja cha radio ambapo alieleza kuwa haweza kumtuma mtu yeyote kuwasambulia mahasidi wake kwa sababu hakuna kitu chochote wataongeza kwa kazi zake.
Ikimbukwe ni mwaka jana ambapo alifunguka kuhusu kilichomfanya kutoka katika lebo ya Wasafi iliyofanya ajulikane kimuziki.
Ambapo alieleza aliyokumbana nayo hasa kwenye kipindi hicho alichokuwa akifanya kazi na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na Msanii Diamond Platinumz.
Konde alisema hayo baada ya kuulizwa na mwanahabari kama huwa anawatuma watu kuzungumza vibaya kwa mahasimu wake.
"Mkiona mtu yeyote anaenda kumzungumzia mtu fulani basi ujue ni maamuzi yake na mimi binafsi siwezi kumtuma mtu yeyote kwa sababu hanisaidii."
Alichukua nafasi hio kupiga vijembe wanaoongea vibaya kuhusu Kikundi chake cha Konde Gang akitaja kuwa wanakiogopa kwa sababu kimeanza kuonyesha ni jinsi gani kinaweza leta ushindani kwenye muziki.
"Ukiona mtu anatuma watu wamzungumzie mtu fulani, basi ujue anawaza kukuhusu" Alisema Harmonize