Harmonize asifia mpenzi wake Briana

Muhtasari

• Akiwa  ziarani nchini Marekani, mwishoni mwa mwezi Novemba, 2021 , alingia kwenye mahaba mazito na mrembo kutoka  Austria

• Hivi majuzi Harmonize  alitania mashabiki wake kwamba wameachana na  kipenzi chake cha roho, Briana. jambo  ambalo  alikuja kueleza ilikuwa uwongo

• Baada ya Briana kuzuru Tanzania, Harmonize alimpeleka moja kwa moja kwa wazazi wake kumtambulisha rasmi, mkoani Mtwara

Harmonize na Briana
Harmonize na Briana
Image: hisani

Ni miezi  miwili imepita tangu mwanamuziki kutoka Tanzania, Harmonize kumtambulisha hadharani mpenzi wake Briana.

Harmonize, akiwa  ziarani nchini Marekani, mwishoni mwa mwezi Novemba, 2021 , alijipata  kwenye mahaba mazito na mrembo kutoka  Austria.

Alipotua  uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere aliwaahidi  mashabiki wake kwamba mwaka ujao, yaani 2022, atafunga ndoa naye.

Hivi majuzi Harmonize  alitania mashabiki wake kwamba wameachana na  kipenzi chake cha roho, Briana, jambo  ambalo  alikuja kueleza ulikuwa uwongo.

Baada ya Briana kuzuru Tanzania, Harmonize alimpeleka moja kwa moja kwa wazazi wake kumtambulisha rasmi, mkoani Mtwara.

Harmonize kwenye kituo kimoja cha runinga ameeleza  kuwa anapanga kuasi ukapera mwaka huu na  anapania kumwalika Ali kiba kutumbuiza kwenye harusi yake.

 

 “Briana ndiye mwanamke wa maisha yangu!” alisema Harmonize.

Briana ni mwanamke wa pili mwenye asili ya kizungu kuwa kwenye uhusiano na Harmonize baada ya kuachana Sarah Michelloti  raia wa Italia.