Sokwe mkongwe zaidi duniani afariki 'kutokana na Covid'

Muhtasari

• Alitambulika kwa jina  la Ozzie, alifariki akiwa na miaka 61  katika jimbo la Atlanta nchini Marekani.

• Nyani huyo mzee aligunduliwa kuambukizwa Corona mwaka jana, na inakisiwa  kuwa ugonjwa huo umekuwa chanzo kikuu cha kifo chake.

Sokwe mkongwe duniani
Sokwe mkongwe duniani
Image: facebook/ zoo atlanta

 Sokwe ndume mwenye umri mkubwa zaidi duniani ametangazwa kufariki katika jimbo la Atlanta nchini Marekani.

Sokwe huyo alitambulika kwa jina  la Ozzie, alifariki akiwa na miaka 61.

Nyani huyo mzee alitambuliwa kuwa miongoni mwa nyani waliopimwa na  kupatikana na COVID-19 mwaka jana, na inakisiwa  kuwa ugonjwa huo umekuwa chanzo kikuu cha kifo chake.

Kupitia ukurusa wa TMZ wameleeza kwamba Ozzie alipatikana  amekufa katika chumba chake cha kulala, Atlanta, siku Jumanne.

Mkuregenzi Mtendaji wa makao alimoishi Ozzie Raymond B, alisema waligundua kuwa afya ya  Ozzie ilikuwa inadorora tangu alipogunduliwa kuwa na virusi vya Covid-19.

 "Ingawa tulijua wakati huu ungefika siku moja, kujua huko hakukufanya chochote kuzuia huzuni kubwa tunayohisi kwa kumpoteza Ozzie," alisema Richard B.

Kulingana na FOX5 huko Atlanta, wafanyakazi  wa mbuga waligundua Ozzie alianza kupoteza hamu ya kula wiki iliyopita -- lakini waliendelea kumtunza na kumtia moyo kula na kunywa.