Mungai Eve afikisha views 70m YouTube, awashukuru mashabiki

Muhtasari

• Mwanablogu Mungai Eve amewashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kutinga views milioni sabini katika mtandao wa Youtube ndani ya mwaka mmoja.

• Mungai ameonekana kuwa mwenye furaha nyingi kwa hatua aliyofanikiwa kuipiga kwa kipindi kifupi huku shukran nyingi zikiwaendea wale wote ambao waliaminia kazi yake na kumpa sapoti tangu siku ya kwanza

instagram KWA HISANI
instagram KWA HISANI
Image: mungai eve

Mwanablogu Mungai Eve amewashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kutinga views milioni sabini katika mtandao wa Youtube ndani ya mwaka mmoja.

Kupitia ujumbe alioachia katika ukurasa wake wa Instagram, Mungai ameonekana kuwa mwenye furaha nyingi kwa hatua aliyofanikiwa kuipiga kwa kipindi kifupi huku shukran nyingi zikiwaendea wale wote ambao waliaminia kazi yake na kumpa sapoti tangu siku ya kwanza.

“Habari ya asubuhi ndugu zangu, ahsante sana kwa kuniwezesha kutinga views milioni sabini kwenye youtube ndani ya mwaka mmoja nashukuru sana,” aliandika MUngai Eve.

Aidha mwanablogu huyo amesema sasa analenga kufikisha views milioni mia moja na subscribers laki tano.

Mungai katika siku za hivi karibuni amezidi kuwahakikishia mashabiki wake kwamba atatia bidii zaidi kuhakikisha kwamba anawapa kazi za za kufurahisha macho na masikio.

Mashabiki wamejitojkeza kwa wingi kumpongeza huku wakiahidi kumsapoti mpaka wakati atakapotimiza ndoto hiyo.