Mahaba niuwe! Emmy Kosgei amsherehekea mumewe

Muhtasari

• Msanii mashuhuri wa injili kwa lugha ya Kalenjin, Emmy Kosgei hakuachwa nyuma siku ya wapendanao kwani alimlimbikizia sifa sufufu mumewe Mnigeria Anselm Madubuko.

• “Usiku zingine ni kama hizi. @amadubuko napenda sana jinsi unavyonipenda. Nakupenda,” aliandika Kosgei

Emmy-Kosgei-with-bae2-e1469435478572
Emmy-Kosgei-with-bae2-e1469435478572

Msanii mashuhuri wa injili kwa lugha ya Kalenjin, Emmy Kosgei hakuachwa nyuma siku ya wapendanao kwani alimlimbikizia sifa sufufu mumewe Mnigeria Anselm Madubuko.

Mumewe ambaye wanaachana kwa pengo la miaka 20, walioana mwaka wa 2013 kwenye hafla ya harusi iliyofanyika kaunti ya Mombasa miezi michache tu baada ya mwanamme huyo kupoteza mke wake wa kwanza kwa kifo.

Tajiri huyo wa kutokea Nigeria anampenda sana Mkenya Emmy Kosgei na anapenda kumuita kwa jina la Nubian Queen, na katu wawili hao hawaogopi kuoneshana mapenzi yao hadharani kwenye mitandao ya kijamii licha ya pengo kubwa baina ya umri zao.

Emmy Kosgei akimsherehekea siku ya wapendanao, ametundika picha zao kwenye Instagram yake na kufuatisha ujumbe mzuri wa upendo kwa mume wake huku akisema kwamba anapenda sana jinsi mume wake anavyompenda.

“Usiku zingine ni kama hizi. @amadubuko napenda sana jinsi unavyonipenda. Nakupenda,” aliandika Kosgei

Wakenya wamemsherehekea muimbaji huyo aliyetamba kwa vibao kama vile Ategsin na Taunet Nelel na kumtakia kila la kheri katika ndoa yake nchini Nigeria huku wengine wakifanya mzaha wao kwa kumuuliza kama huyo mumewe ana ndugu mdogo ili wakaolewe naye pia.