Watu wanajiua kwa unyongovu, wanaomba msaada mnawacheka - Huddah

Muhtasari

• Huddah amesema kwamba watu wamekuwa wanafiki wanaozidi kusema unyongovu ni kweli ila wanapoombwa msaada na wale wenye tatizo hilo, huwageuka na kuwacheka.

Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: Hisani

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Huddah Monroe anasikitishwa jinsi ambavyo huku nje watu wanajivalisha Ngozi ya kondoo kumbe ndani ni umbwa mwitu ambako wanazidi kusema ungongovu na msongo wa mawazo ni jambo la kweli tu bila kuwasaidia wale wanaowafuata kwa ukaribu kuwaomba msaada.

Akiandika kwenye instastories zake, Huddah anasikitika jinsi ambavyo watu wanatia huruma huku nje wakati mwenzao amekufa kwa kujiua kutokana na unyongovu na kusema kwamba wengi wa hao wqanaotia huruma mara nyingi wanafuatwa na waathirika kwa msaada ila wanachokifanya ni kuwacheka, kuwakejeli, kuwachamba mitandaoni na kisha kuwakwepa kabisa.

“Inachekesha sana jinsi ambavyo watu huku nje mmejaa mkisema kwamba unyongovu ni kweli. Wale watu ambao hujiua kwa unyongovu na msongo wa mawazo, ni wangapi mnaowajua binafsi na ambao waliwafuata kutaka msaada wenu, lakini mlichokifanya ni kuwakebehi na kuwakwepa? Mshindwe huku nje mnaoigiza kutia huruma,” aliandika Huddah Monroe.

Hivi majuzi akimuomboleza rapper wa Afrika Kusini aliyejiua, Huddah alizua mjadala kwamba wasanii wengi wanaonekana wako sawa katika muonekano wa nje ila ndani wanapambana usiku na mchana katika vita na nafsi zao na msongo wa mawazo kwa sababu hawana mtu wa karibu nao ambaye wanaweza kufunguka kuhusu kile kinachowasibu maishani mwao.