Madee na Roma Mkatoliki wataniana kuhusu kirefu cha #FOA

Muhtasari

• Wasanii wa hiphop nchini Tanzania wamesisimua mtandao wa Twitter baada ya kuendeleza msururu wa kutaniana kuhusu kirefu cha EP ya Diamond Platnumz.

Madee, Roma Mkatoliki
Image: Twitter

Wasanii wa hiphop nchini Tanzania Madee na Roma Mkatoliki wanazidisha utani wao kwenye mtandao wa Twitter kwa kurushiana vijembe utadhani wana uhasama kumbe ni matani yao tu na safari hii utani umerejea tena baina yao huku wakibishania kirefu cha jina la EP ya Diamond Platnumz.

Wawili hao wamekuwa katika utani wa muda mrefu ambapo kila mara wanataniana kwenye mtandao wa Twitter kuhusu matukio mbalimbali ya nchini Tanzania na bara la Afrika ambapo safari hii wametua kwenye kilele cha #FOA.

Madee ndiye aliyeanzisha utani huo kwa kuweka picha ya Roma Mkatoliki kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika #FOA na mabanoni akasema kwamba maana yake ni haraka kuondoka Marekani kwa rapa Roma.

“Mmarekani wa mchongo nayeye kaona isiwe tabu #FOA anayo..(Faster Ondoka America),” aliandika Madee.

Ikumbukwe Roma Mkatoliki alihamia Marekani miaka michache iliyopitqa kutokana na kuhangaishwa kwake na baadhi ya watu aliowataja kwamba wanampiga vita kutokana na harakati zake za kuuponda uongozi wan chi katika nyimbo zake.

Roma pia hakusita kwani utamu wa utani ni majibizano na kadri yanavyozidi kukoleqa basi ndio utani nao unaendelea kunoga.

“Fala Ondoka Afrika,” alijibu mipigo Roma huku akiwa amepakia picha ya Madee.

Utani huu ulisisimua kwenye mtandao wa Twitter huku wengi waliendeleza gumzo la utani baina ya wawili hao ambapo baadae Diamond alikuja kutoa maana halisi ya #FOA  na kusema kwamba ina maana ya Kabla ya Yote yaani ‘First of All’