Ringtone atoa ahadi ya 1M kwa Diana Marua amtafutie mke

Muhtasari

• Msanii wa miziki ya injili, Ringtone Apoko amesema kwamba yupo radhi kutoa shilingi milioni moja kwa Diana Marua ili amtafutie mchumba.

• “Diana najua wewe una rafiki wengi warembo, basi tumalize haya maneno, nitafutie mmoja nimuoe,” Apoko alisema.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Ringtone Apoko

Msanii wa miziki ya injili, Ringtone Apoko amesema kwamba yupo radhi kutoa shilingi milioni moja kwa Diana Marua ili amtafutie mchumba.

Akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha #CookAnd Reveal, Ringtone alisema kwamba anataka mmoja kati ya rafiki zake Marua awe mchumba wake, akisema kwamba hilo litarahisisha mchakato wake wa kutafuta mke.

“Diana najua wewe una rafiki wengi warembo, basi tumalize haya maneno, nitafutie mmoja nimuoe,” Apoko alisema.

Ringtone alitoa hakikisho la kumtunza mpenzi wake, na kwamba atatoa mazingira mazuri ya ndoa yao kunawiri.

Aidha alisema kwamba angependa sana kupata mke ambaye atakumbatia upungufu wake na kasheshe zake katika mitandao ya kijamii.

Kwa muda mrefu sasa Apoko amekuwa akitafuta mke bila mafanikio, huku akishikilia kwamba atazidi kusaka mpaka atakapopata Yule anayeandana na matakwa yake.

Apoko ni moja kati ya wasanii ambao wanajituma katika kazi zao za kimuziki, na pia kutoa tumaini kwa chipukizi ambao wangependa kuingia katika sekta ya burudani.