Acheni kunila kwa macho! Ringtone awaonya wanawake

Muhtasari

• Mwimbaji Ringtone amewataka wanawake wakome kumla kwa macho na kusema kwamba yeye ni mtoto wa Mungu.

Ringtone Apoko
Image: Instagram

Msanii wqa injili mwenye utata Ringtone Apoko hakosi jipya kila siku ya Mungu, kutoka kujishaua mitandoni jinsi alivyotajiri, kupatikana kwa visa, visangqa na Mikasa na kuwashambulia wasanii wenziwe kwa cheche kali. Mwanamuziki huyo ambaye alijitangaza kama mwenyekiti wa wasanii wa injili nchini Kenya safari hii amekuja na jipya ambapo kombora lake limeelekezwa kwa wanawake ambao anasema wanamkodolea macho kwa sababu ya uzuri alio nao eti.

Kwenye Instagram yake, Ringtone amepakia picha yake na kuandika onyo kali tena kwa herufi kubwa akiwakanya wanawake kukoma kumla kwa macho kwani yeye ni mtoto wa Mungu.

“Wanawake, acha kunila kwa macho tafadhali, mimi ni mtoto wa Mungu,” ameandika Ringtone.

Licha ya kujulikana kwa mzaha wake wa kuboronga Kiingereza, watu wengi wamefurika kwenye ukurasa huo na kumkejeli kwa kusema kwamba wanawake wanamla kwa macho.

“Wee nawe usitukule kichwa,” mmoja aliandika.

“Una mzaha sana, unafaa ubadilishane majukumu ya uigizaji na Eric Omondi. Wewe ni mcheshi,” mwingine aliandika.