Arrow Bwoy kumnunulia Nadia Mukami gari na shamba?

Muhtasari

• Msanii Arrow Bwoy amesema kwamba atamnunulia mke wake gari ama shamba atakapojifungua.

“Nadia nimetoka mbali sana naye, niko tayari kufanya chochote kwa npenzi wangu,” Arrow Bwoy alisema.

Arrow Bwoy
Arrow Bwoy
Image: instagram/AB

Msanii Arrow Bwoy amesema kwamba atamnunulia mke wake gari ama shamba atakapojifungua.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini, Arrow alisema kwamba yupo tayari kufanya chochote maadamu mke wake, Nadia Mukami afurahie.

“Nadia nimetoka mbali sana naye, niko tayari kufanya chochote kwa npenzi wangu,” Arrow Bwoy alisema.

Alitoa himizo kwa wanaume wote kuwanunulia wake zao zawadi kama njia moja ya kuwashukuru kwa kazi nzito ya kubeba mimba na kujifungua.

Aidha alisema kwamba walipoteza mtoto wao wa kwanza, hali ambayo iliwapelekea kuanzisha wakfu wa Lola na Safari ili kusaidia kina dada ambao wanapata changamoto katika safari ya uzazi.

Alikiri kwamba kuna wakati ambapo wamekosana na Mukami kutokana na mhemko wa hisia unaoletwa na mimba.

Arrow Bwoy alisema kwamba yupo tayari kumkaribisha mtoto wao na kwamba atajituma kuhakikisha anampa maisha mazuri.

Alizungumza haya wakati ambapo anajiandaa kuachia album yake ya #Focus tarehe 12/3/2022, akisema kwamba Nadia Mukami, Sanaipei Tande , Nandy ni miongoni mwa wasanii waliohusishwa katika album hiyo.