Diamond Platnumz asema anamheshimu sana Alikiba

Muhtasari

• Diamond Platnumz akiri kuwa na heshima kwa staa wa bongo Alikiba.

• Alisema kwamba mashabiki wameishi kuwapiganisha jambo ambalo kwake ni ushamba tu.

Diamondplatnumz
Diamondplatnumz
Image: Instagram KWA HISANI

Mwanamuziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz amekiri wazi kwamba anamkubali msanii mwenzake Alikiba na hajawahi kuwa na ugomvi naye.

Amesema anamheshimu Alikiba kwa kufanikiwa kudumu kwenye gemu la burudani kwa muda mrefu.

Platnumz alikiri kwamba alikuwa akiumizwa sana na ugomvi uliokuwa unajengwa kati yao na mashabiki, kwani lilisambaratisha mazingira ya kushirikiana kwenye kazi.

Simba pia alisema kuna kipindi Ali alimpata studioni na kumuomba wafanye kibao ila Alikiba alionekana kutokuwa tayari kumpa shavu kwenye muziki  huo.

Alisisitiza kwamba mara kadhaa ashawahi kumualika Alikiba katika hafla zake nyingi ila hakuhudhuria.

Alishikilia kwamba anachokichukia ni watu kujaribu kumwangusha akisema kwamba yeye ni msanii mkubwa na mkali, kwa hiyo kumfanya afeli ni vigumu sana.

Kwa sasa Diamond anazidi kupromote EP yake ya  #FOA ikisubiriwa kuona mashabiki wataikubali kiasi gani.