'Sina tatizo na Alikiba,'Diamond afichua kilichochochea ugomvi wake na Alikiba

Muhtasari
  • Diamond alidai kwamba ni kama Alikiba hakuwa tayari  kufanya collabo ya  kibao hicho
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Diamond Platinumz

Staa wa bongo Diamond Platnumz amesema kwamba hana tatizo lolote na msanii Alikiba, hata baada ya uvumi kuende kwamba wana ugomvi.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Fm, alisema kwamba alitaka kufanya collabo na Alikiba katika kibao chake cha 'Lala salama'.

Diamond alidai kwamba ni kama Alikiba hakuwa tayari  kufanya collabo ya  kibao hicho.

Zaidi ya yote Diamond amedai kwamba hana shida na mtu yeyote licha ya uvumi wa kuwa na ugomvi naye.

"Nilikuwa Nataka Tufanye Nyimbo, So Akanikuta Studio Kwa KGT Ambaye Alikuwa Producer Wake, Ni Kwambia Tufanye Wimbo, ...nikamchezea #LalaSalama, Nikasema Naweza Kufuta Verse Ya Pili Halafu Ukaingiza Yakwako Akawa Na Anasema Ah !

Sa Mi Nadhani Sijui Hakuwa Tayari Kwenye Kufanya Verse Alichofanya Akafanya adlibs, Hasa Kwenye Nyimbo Kufanya Adlibs Za Juu Haifai,

Hata Shabiki Yako Akisikia Atakuonaje, Kwahiyo Hakufanya Verse Nikaona Bora Nifanye Mwenyewe Sasa, Kwasababu Mi Niiitaka Afanye Verse ...Ila Trust Me Sina Shida Na Mtu Yeyote."