Diamond awataka wasanii wa Tz kutoshindana wao kwa wao

Muhtasari

• Diamond amewataka wasanii wa Bongo kukoma kujihusisha na vita vya wao kwa wao.

• ''Kunatakiwa kuwe na wivu wa kimaendeleo unaongeza kasi kwa sababu wale wenzatu wana hasira sana na dunia lakini unakuta kuna watu wana hasira na Diamond,” Simba alisema.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Diamond Platinumz

Msanii kutoka Tanzania, Diamond Platinumz ametoa ombi kwa wasanii na mashabiki kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na badala yake kutafuta mbinu mbadala kushindana na wasanii wa kimataifa.

Akizungumza katika mahojiano ndani ya Wasafi fm, Simba alisema kwamba Bongo ina vipaji vingi tena vikali ila vinaishia kutofanya vizuri kwa sababu ya fitina vya wao kwa wao vinavyoletwa na mashabiki ama wasanii wenyewe.

Diamond alisisitiza kuwa wasanii wanapaswa kufanya juhudi zaidi kupata hela kutokana na vipaji vyao wala sio kutafutiana ugomvi usio na manufaa.

''Kunatakiwa kuwe na wivu wa kimaendeleo unaongeza kasi kwa sababu wale wenzatu wana hasira sana na dunia lakini unakuta kuna watu wana hasira na Diamond,” Simba alisema.

Kauli ya Diamond inajiri siku chache baada ya kuachia EP yake #FOA, ambayo inazid kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali za kimuziki pale Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wengi wa mashabiki pia wanahisi maneno ya Mondi yanajiri baada ya mashabiki kwa muda mrefu kumlinganisha na Harmonize na Alikiba.