EP ya Diamond ilichaguliwa kutoka kwa vibao 200 - Babalevo

Muhtasari

• Msanii Babalevo ameweka wazi kwamba EP yake Diamond Platinumz ilitokana na asilimia ndogo tu ya vibao zaidi ya 200 ambavyo mwanamuziki huyo bado hajaachia.

• Alitaja kwamba Simba ni msanii mkubwa ambaye amechangia pakubwa katika harakati za kukuza muziki wa Bongo, na kwamba anapaswa kupewa heshima yake.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Babalevo

Msanii Babalevo ameweka wazi kwamba EP yake Diamond Platinumz ilitokana na asilimia ndogo tu ya vibao zaidi ya 200 ambavyo mwanamuziki huyo bado hajaachia.

Akizungumza katika mahojiano na Samissago, Babalevo alikiri kwamba hicho kilikuwa kionjo cha kazi nyingi ambazo Simba atakuwa anatoa.

“Hiyo EP ya FOA imetolea kwa nyimbo 200 alizonazo. Amezichambua akaona hizi acha niwapelekee mashabiki wangu,” alisema Babalevo.

Aidha Babalevo alisema kwamba atakuwa akiwaelezea mashabiki kila hatua ya maisha ya Diamond Platinumz kama njia moja ya kuonyesha kwamba yeye ni msanii mkubwa kupitia mambo anayoyafanya.

Aliongezea kwamba tayari Diamond alikuwa katika taifa la Nigeria ambapo alirekodi video nne za muziki ambazo zipo nje ya EP.

Alitaja kwamba Simba ni msanii mkubwa ambaye amechangia pakubwa katika harakati za kukuza muziki wa Bongo, na kwamba anapaswa kupewa heshima yake.