Zuchu afutilia mbali madai ya ugomvi na mamake Diamond

Muhtasari

• Zuchu aliweka wazi kuwa uhusiano wake na Mama Dangote ungali mzuri.

Zuchu na Mama Dangote
Zuchu na Mama Dangote
Image: INSTAGRAM

Malkia wa muziki wa Bongo Zuhura Othman almaarufu Zuchu amekanusha madai kuwa kuna beef kati yake na mama ya Diamond, Bi Sanura Kassim (Mama Dangote).

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Zuchu aliweka wazi kuwa uhusiano wake na Mama Dangote ungali mzuri.

Alisema kuwa bado wanafuatiliana kwenye mitandao ya kijamii, kinyume na tetesi ambazo zimekuwepo kuwa Mama Dangote aliacha kumufollow Instagram baada yao kutofautiana.

"Sio kweli. Nadhani wametengeneza ile. Mama Dangote amenifollow nami pia nimemufollow. Hakuna shida yoyote. Hajawahi kunikosea  na sijawahi kumkosea kwa lolote. Hakuna shida.Watu wanatengeneza vitu tu," Zuchu alisema.

Siku za hivi majuzi kumekuwa na uvumi kuwa hakujakuwepo na maelewano mazuri kati ya Zuchu na mama huyo wa bosi wake.

Screenshots zinazoonyesha kama kwamba wawili hao wameacha kufuatiliana kwenye mtandao wa Instagram zimekuwa zikisambazwa kuunga mkono tetesi hizo.