Arrow Bwoy amefichua kwamba wanatarajia mtoto wa kiume

Muhtasari

• Licha ya kuchanganya watu na rangi ya nguo walizozivalia wakati wa kutangaza ujauzito wao, Arrow Bwoy amebainisha wazi kwamba mtoto anayetarajiwa ni wa kiume.

• Siku ya kutangaza ujauzito huo, walivalia nguo rangi ya pinki inayoashiria mtoto wa kike.

Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAMI

Msanii Arrow Bwoy ameweka wazi kwamba yeye na mpenzi wake Nadia Mukami wanatarajia mtoto wa kiume, siku chache tu baada ya wawili hao kuweka wazi juu ya ujauzito wa Nadia.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee katika kituo kimoja cha redio nchini, Arrow Bwoy alitetea hatua ya rangi za nguo walizozichagua ambazo zinaashiria ujauzito ni wa mtoto wa kike.

Aliulizwa kwamba mbona waliamua kuvalia nguo za rangi ya pinki wakati wanaweka wazi habari za ujauzito wa mpenzi wake Nadia. Wajuzi wa rangi wanasema rangi ya pinki wanahoji rangi hiyo aghalabu huashiria mtoto wa kike.

Arrow Bwoy alisema kwamba hawakuwa wanajua jinsia ya mtoto kwa sababu ilikuwa kama jambo la kushtukiza na ambapo pia walipata kufahamu jinsia ya kijajo hiyo siku wakiweka wazi habari njema ya ujauzito wa mpenzi wake.

Kwa kawaida habari za mimba ya mtoto wa kike huwa ni pinki huku yule wa kiume kiashiria chake kikiwa ni utaradadi wa rangi za samawati au nyekundu.

Msanii huyo pia alisema kwamba majina wa wakfu wao ambao waliuzindua siku hiyo kwa jina Lola na Safari yalitokana na majina waliyokuwa wamekusudia kumuita mtoto wao wa kwanza ambaye kwa bahati mbaya mimba hiyo iliharibika hata kabla hawajajua jinsia.

Aidha alisema kwamba yeye kwa upande wake kama mwanaume alikuwa amebashiri mtoto atakuwa wa kike huku mpenzi wake Nadia akibashiri mtoto atakuwa wa kiume, na ndio hivo mwisho wa siku Nadia akagonga ndipo.