Arrow Bwoy asema anafurahi sana kuwa baba

Muhtasari
  • Mapema wiki msanii Nadia Mukami na Arrow Boey walifichua kwa wanamitandao kwamba wanatarjia mtoto wao wa kwanza
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Nadia Mukami na Arrow Bwoy

Mapema wiki msanii Nadia Mukami na Arrow Boey walifichua kwa wanamitandao kwamba wanatarjia mtoto wao wa kwanza.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini, Arrow alisema kwamba yupo tayari kufanya chochote maadamu mke wake, Nadia Mukami afurahie.

Pia msanii huyo akiwa kwenye mahojiano hayo siku ya Ijumaa alisema kwamba anafurahi sana kuwa baba.

Arrow alisema walihuzunishwa sana na kufiwa na mtoto wao wa kwanza baada ya Nadia Mukami kuharibikiwa na mimba.

"Nimefurahi sana kuwa baba. Tulipanga kwa hilo." "

Akizungumzia kuharibika kwa mimba kwao hapo awali, msanii huyo alishiriki

'Ilimpata kwa mshangao ndipo tukaamua kukumbatia, Tulikuwa tumwite mtoto Lola na Safari.

Tulianza kutafuta mtoto mwingine kwa moto kwa nguvu, kwani tulikuwa tumeanza kuwapenda watoto."