(Video) 'Tumepitia mengi sana,' Hatimaye Arrow Bwoy amvisha Nadia Mukami pete ya uchumba

Muhtasari

•Wapenzi hao walicheza ngoma kadhaa pamoja na katika kilele cha matumbuizo yao kitu kizuri kilipendeza, Arrow Bwoy alipiga goti na kutuma posa kwa kipenzi chake Nadia.

•Nadia ambaye alionekana kuwezwa na hisia za furaha alisongea karibu na baba huyo wa mtoto ambaye amebeba na kumkumbatia.

Image: INSTAGRAM//NADIA MUKAMI

Jumamosi ya Machi 13, 2022 ilikuwa siku maalum sana kwa wasanii na wapenzi mashuhuri Arrow Bwoy na Nadia Mukami.

Arrow Bwoy ambaye amekuwa akitumbuiza kwa miaka mingi alizindua albamu yake mpya inayoitwa 'Focus' katika jukwaa la Junction Mall, jijini Nairobi.

Hafla ya uzinduzi wa albamu ya Arrow Bwoy  ilihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walishuhudia matumbuizo ya moja kwa moja kutoka kwa wasanii kadhaa ambao walikuwemo.

Licha ya kuwa mjamzito, Nadia alihudhuria hafla hiyo maalum kwa mumewe na kutumbuiza kwa ngoma kadhaa pia.

Wapenzi hao walicheza ngoma kadhaa pamoja na katika kilele cha matumbuizo yao kitu kizuri kilipendeza, Arrow Bwoy alipiga goti na kutuma posa kwa kipenzi chake Nadia.

"Sijui  niseme nini. Tumepitia mengi sana. Watu wamebonga sana. Wengine hawajaamini hadi wa leo yani.Nakupenda sana na ningependa kuishi maisha yangu yote nawe. Mpenzi wangu mrembo zaidi, mbele ya umati huu wote, je utakubali tufunge ndoa?" Arrow Bwoy alisema baada ya kupiga goti.

Nadia ambaye alionekana kuwezwa na hisia za furaha alisongea karibu na baba huyo wa mtoto ambaye amebeba na kumkumbatia.

Baada ya hayo alijibu 'Ndio' na Arrow Bwoy hakusita kumvisha mpenzi huyo wake wa kipindi kirefu  pete ya uchumba.

Tazama video»»»

Mashabiki waliohudhuria hafla hiyo waliwatakia wawili hao mema katika ndoa yao.

Hivi majuzi Arrow Bwoy akihutubia waandishi wa habari wakati wa matayarisho ya uzinduzi wa albamu yake aliapa kuwa lazima angemuoa Nadia.