Marioo adokeza kufanya Mi Amor 'remix' na Davido

Muhtasari

• Marioo alidokeza kwenye instagram yake kwamba wanatazamia kuachia remix ya collabo ya Mi Amor na staa kutoka Nigeria, Davido.

Marioo na msanii Davido
Marioo na msanii Davido
Image: INSTAGRAM

Msanii Marioo kutoka Tanzania ametangaza kwamba hivi karibuni mashabiki wake watarajie kusikia ‘remix’ ya collabo yake na msanii kutoka Kenya, Mi Amor.

Akiandika kwenye Instagram yake, Marioo alidokeza kwamba wanaendelea kuishughulikia ‘remix’ hiyo ambayo safari hii wanamshirikisha mkali wa hizo shughuli kutoka Nigeria, Davido.

“Mi Amor remix ft OBO, au basi achene tu,” aliandika Staa huyo wa bongo, Marioo.

Ngoma hiyo ya Mi Amor imekuwa ikifanya vizuri na kupata ufanisi mkubwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kupakua miziki ambapo kwa nchini kenya tu, imekuwa ikidedea kileleni mwa chati za muziki kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Ikumbukwe hii ndio ngoma ambayo mfalme wa bongo fleva Diamond Platnumz aliisikiliza na kuipungia mkono sana ambapo mpaka ilimbidi kuipakia kwenye instastories zake kwa kipindi kimoja huku akiwaomba watu wakaitizame.

Hili lilikuwa tukio muhali kwelikweli ambapo lilizua mijadala mitandaoni kuhusu hatua hiyo kwani wengi wanamjua Diamond si mtu wa kusukuma kazi za wasanii kutoka nje ya rekodi lebo yake ya Wasafi na hili lilitokea kama mshangao kwa wengi.

Ngoma hiyo kwa sasa ina watazamaji zaidi ya milioni 4.3 kwenye mtandao wa YouTube katika wiki nne tangu video ya dude hilo kutolewa.