Marioo atamba kwenye chati za muziki Kenya

Muhtasari

• Ngoma mpya ya Marioo inazidi kutesa anga katika sanaa ya muziki nchini Kenya baada ya kuibuka ya kwanza katika orodha ya ngoma bora pendwa za wiki nchini Kenya.

Marioo
Image: Facebook

Chati za muziki wa nchini Kenya za wiki hii ya mwisho wa mwezi Februari zimetolewa na kwa kweli wasanii wa Kenya wanazidi kukaza buti na kuwakilisha vilivyo ila bado kazi ipo ya kuifanya ili kuufikia muziki wa bongo.

Kwenye orodha ya ngoma ishirini bora za wiki nchini Kenya, ngoma inayoshikilia nafasi ya kwanza ni ile ya Msanii Marioo akimshirikisha msanii wa Kenya Jovial ambaye hivi amjuzi ametangaza kwamba amefunga ukurasa wa kufanya collabo tena na wasanii wengine.

Ngoma hiyo kwa jina Mi Amor ambayo video yake imetolewa takribani wiki mbili zilizopita inashikilia nafasi ya kwanza kutokana na ueledi wa mistari na vina katika utunzi wake.

Ikumbukwe ngoma hii si Kenya tu ambapo imeibuka ngoma pendwa bali hata nchini Tanzania video yake ilipotoka ngoma hiyo ilishabikiwa pakubwa na wengi akiwemo gwiji wa mambo hayo, Diamond Platnumz mwenyewe ambaye aliweka kwenye instastories zake akishabikia ueledi wake na kuwasihi wafuasi wake waiangalie kwenye majukwaa yote ya muziki kote ulimwenguni.

Post hiyo ya Diamond iliwaacha wengi wakizungumza haswa ikizingatiwa kwamba Diamond ana mazoea ya kusukuma kazi ya wasanii ambao wamesainiwa chini ya rekodi lebo ya Wasafi lakini safari hii aliisukuma ya msanii Marioo ambaye hayupo pale Wasafi, ila sasa wengi baada ya kuisikiliza ngoma hii walipata kuelewa nini Diamond alikuwa anamaanisha kwa kuisukuma kwani kilichobora hupata uungwaji mkono.

Kwenye orodha hiyo, ngoma ya Nyashinski akimshirikisha rapa Femi One, almaarufu Proper inakuja ya pili na kuidengua ile ya Bien Baraza na Aaron Rimbui ya Mbwe Mbwe ambayo ilishikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Mambo mengine yqa kuzungumziwa kwenye orodha hiyo ni ngoma zilizoporomoka jedwalini kwa kiasi kikubwa ambako collabo ya Nyashinski na Khalighraph Jones ya Sifu Bwana iliyotolewa mwezi Januari mwaka huu ikiporomoka mara tano Zaidi. Vile ville ngoma ya Willy Paul ya Toto pia imefanya vibaya na iko katika hatari ya kudondoka nje ya ishirini bora baada ya kuporomoka mara tano pia nayo Adhiambo ya Bahati na msanii wa benga Prince Indah ikiporomoka mara sita katika viwango vya jedwali hilo.

Je, unahisi ni ngoma gani inafaa kutoka na gani inafaa kuingia kwenye orodha hiyo katika mwezi huu wa Machi?

Image: Instagram